DAR ES SALAAM
Na Nicolaus Kilowoko
Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Yanga, Pedro Goncalves, amefunguka kuhusu umuhimu wa kufanya usajili, kuelekea katika dirisha dogo la usajili, huku matamanio yake makubwa ni kuwa na kikosi chenye ushindani, katika mashindano ambayo wanashiriki msimu huu.
Goncalves alisema kuwa kufanya usajili ndani ya klabu yake, ni jambo zuri ila ataangalia hasa ni maeneo gani ya kufanya maboresho, kwani tayari ameendelea kuwajumuisha wachezaji wote waliosajili msimu huu, katika mechi mbalimbali.