DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Singida Black Stars, imeandaa mkakati wa kuhakikisha katika kipindi hiki cha mapumziko, wanafanya maboresho machache ambayo yalikuwa ndani ya kikosi chao.
Kupitia kwa msemaji wao Hussein Massanza alisema kwamba, kupoteza kwenye mchezo wao dhidi ya TRA United, kumewafanya waone mapungufu mengi ndani ya klabu yao, ambayo kocha wao Miguel Gamond anakwenda kuyafanyia marekebisho.