Mwanza
Na Paul Charles Mabuga
Kichapo cha 2-0 kutoka kwa Azam FC, si tu kwamba kimepunguza kasi ya Simba kwenye mbio za ubingwa, bali kimetupa picha ya kutisha: Simba inaumwa, na wapinzani wamegundua dawa ya ugonjwa wake.
Matokeo haya yanazua swali gumu: Je, timu hii imegeuka kuwa Mnyama wa Karatasi? Uchambuzi huu unakwenda ndani kabisa, ukifichua kwa nini udhaifu mmoja unajirudia, na jinsi benchi la ufundi linavyoshindwa kuleta ufumbuzi, dhidi ya mbinu za kisasa za mpinzani. Hii ni muhimu kwa kuwa timu imefungwa namna ile ile, kama ilivyotokea kwa Stade Malien.