DAR ES SALAAM
Na Arone Mpanduka
Panenka ni mbinu maalumu ya kupiga penati katika mpira wa miguu, ambapo mchezaji hupiga mpira kwa upole na kwa ustadi katikati ya lango, badala ya kupiga kwa nguvu kuelekea pembe za lango.
Mbinu hii inalenga kumshawishi kipa kwenda upande mmoja, kabla ya mchezaji kupiga mpira polepole katikati, hivyo kumfanya kipa ashindwe kufikia mpira.