Dar es Salaam
Na Mwandishi wetu
Meneja wa beki kisiki wa klabu ya soka ya Yanga, Bakari Mwamnyeto, Carlos Sryvester, amekata mzizi wa fitina juu ya hatma ya mteja wake, ambaye kulikuwa na tetesi kuwa, nyota huyo anatarajiwa kuondoka ndani ya klabu hiyo.
Mkataba wa Mwamnyeto na klabu yake ya soka ya Yanga, umemalizika rasmi msimu huu, huku kukiwa bado hakuna mazungumzo yoyote, ambayo mpaka sasa yamefikiwa na pande zote tatu.
Akizungumzia juu ya hatma ya mchezaji huyo, Meneja wake Carlos aliweka wazi kwamba, bado hakuna mazungumzo yoyote, ambayo wameshayafanya na klabu ya soka ya Yanga, juu ya kuongeza mkataba na mchezaji huyo, japo ni kweli amemaliza mkataba wake.