Print this page

Alonso amng’ang’ania Fernandez Chelsea

LONDON, Uingereza
Meneja mpya wa klabu ya soka ya Chelsea, Xabi Alonso, aliyeanza kazi yake Stamford Bridge, ameweka ngumu na kutaka kumbakisha kiungo mshambuliaji, Enzo Fernandez, klabuni hapo.
Kiungo huyo wa kati wa Argentina, mwenye umri wa miaka 25, alikuwa anatakiwa na klabu ya soka ya Real Madrid ya Hispania, kwa bei kubwa ya Pauni milioni 120, lakini Alonso bado ameonesha nia ya kumuhitaji zaidi.
Alonso alikiri wazi kumuhitaji nyota huyo, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari, tangu achukue jukumu la kuiongoza Chelsea, kufuatia kuondoka kwake Real Madrid mnamo Januari.
“Ndio tumezungumza, lakini kama unavyoelewa, tulichosema kitabaki kuwa cha faragha,” alisema Alonso.
Aliongeza kuwa mshambuliaji Nicolas Jackson, atarudi kwenye kikosi wakati wa maandalizi ya klabu ya msimu nchini Australia na Asia, baada ya Bayern Munich, kuamua kutofanya uhamisho wake wa mkopo kuwa wa kudumu.

Rate this item
(0 votes)
Japhet