Print this page

Waziri Mkuu awataka Watumishi wa Umma kuthamini huduma yao

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watumishi wa Umma kote nchini, watambue na wathamini nafasi za kazi walizonazo, kwamba ni huduma wanazotakiwa kuzitoa kwa wananchi.
“Ninapokuwa kwenye hizi ziara, nimekuwa ninawaambia watumishi wenzangu walioko maofisini kwamba, kuwa kwenye hizi nafasi ni huduma, ni utumishi, na kuwazungusha watu wanapotaka hizo huduma ni ushamba,” alisema.
Waziri Mkuu alitoa wito huo Ijumaa, Juni 05, 2026, wakati akizungumza na wakazi wa Jimbo la Isimani, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kijiji cha Isimani, Kata ya Kihorogota, Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa.
“Tutahakikisha hoja zote zinazotolewa na wananchi zinafanyiwa kazi, kwa sababu huo ndio wajibu wa Serikali, kuwatimizia wananchi yale yaliyo mahitaji yao ya kila siku, ili waweze kufanya kazi wakiwa na utulivu. Nitoe rai kwa ofisi zote za umma, tuyazingatie hayo,” alisisitiza.

Rate this item
(0 votes)
Japhet