Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Henry Mchamungu (wa tatu kushoto) akiwa katika maandamano na Waamini wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma - Mbezi Beach, Jimboni humo wakati wa sherehe za Sikukuu ya Ekaristi Takatifu baada ya adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu iliyoadhimishwa Dominika iliyopita parokiani hapo. Aliyebeba Monstranti yenye Ekaristi Takatifu ni Padri Rogatian Msafiri Paroko wa Parokia hiyo.