Print this page

Zilizala la Maandishi ya Bajaji: Gazeti la siri linalotembea barabarani

By December 12, 2025 43 0

Mwanza

Na Paul Mabuga

Maandishi yaliyoandikwa kwenye bajaji zetu, ambayo  kwa  muhtasari na kwa  muktadha wa yaliyokusanywa katika makala haya, unaweza kusema ni kama kutoka, “Enzi za Mwalimu” hadi “Kwenye Ndoa Yenu...”:, na vilevile ni maneno yanayosema mengi yenye kusisimua, kuibua hisia, kufurahisha na hata kufikirisha, sembuse kutia hofu na kuogofya.

Ni kwamba licha ya barabara za miji yetu hapa nchini, kujaa watu na shamrashamra za kelele za honi, lakini  pia zimesheheni  falsafa ya Mswahili.. Sio kwenye vitabu au kwenye mikutano ya hadhara, bali kwenye mabango madogo yaliyobandikwa, au kuandikwa nyuma ya magari yetu ya usafiri, na vyombo vingine maarufu kama Bajaji.

Rate this item
(0 votes)
Japhet

Latest from Japhet