Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Baadhi ya Vijana waimarishwa katika Parokia ya Watakatifu  Wote Kiluvya, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

Paroko wa Parokia ya Watakatifu Wote Kiluvya Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Justus Rugaimukamu, akiwabariki waamini waliotoa Zaka wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara parokiani hapo hivi karibuni. (Picha na Yohana Kasosi)

Baadhi ya Vijana walioimarishwa kwa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara katika Parokia ya Mtakatifu Andrea Mtume, Bahari Beach, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (katikati) na Padri Danipaso Bitegeko, Paroko wa Parokia ya Watakatifu Wote Kiluvya (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Mzee Tumaini Makwesa, baada ya Adhimisho la Sakramenti ya Kipaimara parokiani hapo hivi karibuni. (Picha na Yohana Kasosi)

Wanaume Katoliki Uwaka wa Parokia ya Mtakatifu Dominico, Mbezi Juu Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Uwaka Day parokiani hapo hivi karibuni. (Picha na Yohana Kasosi)

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, Mhashamu Simon Masondole, Mapadri, Viongozi wa Halmashauri ya Walei Parokia na Kigango, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo (kushoto kwa Askofu), baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, sanjari na Harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kigango cha Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Kilimahewa Juu, Parokia ya Mtakatifu Agostino – Salasala, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. (Picha na Mathayo Kijazi)

Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu kwenye viwanja vya Seminari ya Mtakatifu Maria, Visiga-Kibaha mkoani Pwani walipopeleka majitoleo yao kuwategemeza Waseminari. (Picha na Michael Ally)

Vijana wa Parokia ya Mtakatifu Nicholaus – Kunduchi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika maandamano ya kuingia kanisani kwa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara. (Picha na Mathayo Kijazi)

Kwaya Shirikisho ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiimba wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu shukrani kwenye viwanja vya Seminari ya Mtakatifu Maria, Visiga-Kibaha jimboni humo walifanya hija ya kuitegemeza Seminari hiyo.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (aliyeshika fimbo ya kichungaji) akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri, Sista mlezi, Viongozi wa Parokia na watoto waliopokea Komunio ya Kwanza katika Parokia ya Mtakatifu Andrea Mtume, Bahari Beach jimboni humo. Kushoto kwa Askofu ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Marco Loth. (Picha zote na Yohana Kasosi)