Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Bukoba

Na Mwandishi wetu

Balozi na Mwanadiplomasia wa Vatican, Mhashamu Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ambaye ni Mtanzania, amefariki Dunia Jumanne ya Septemba 16, mwaka huu mjini Roma nchini Italia.
Taarifa iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Jovitus Mwijage  kwa Maaskofu, Mapadri, Watawa na Waamini ilieleza kwamba Askofu Mkuu Rugambwa aliaga Dunia wakati akipatiwa matibabu kutokana na changamoto za kiafya.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Wakristo wametakiwa kuwa na misalaba katika nyumba zao, iwasaidie kumshinda shetani pale anapowakaribia.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, alitoa siri hiyo hivi karibuni wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na utoaji wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa vijana 52, katika Parokia ya Mtakatifu Maurus - Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Mbozi

Na Mwandishi Wetu

Katika hatua muhimu ya kupunguza upofu, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) na Shirika la Helen Keller International, leo wamewasili mkoani Songwe kwa ajili ya kutoa Huduma Mkoba ya matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho “Cataract Management”, kwa wananchi takribani 700 wa Songwe, katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi (Vwawa).
Akiongea na Waandishi wa Habari, Dk. Jofrey Josephat Mratibu wa Huduma za macho Mkoa wa Songwe, alieleza kuwa kambi hiyo ya siku sita imelenga kukabiliana na magonjwa ya mtoto wa jicho, na kusogeza huduma hizo adimu katika maeneo ya karibu na wanapoishi (vijijini), ambapo imekuwa ngumu kupatikana na gharama kwa wananchi, kuzifuata katika hospitali kubwa.

Mwanza

Na Mwandishi Wetu

Simanzi imetawala katika Kanisa Katoliki nchini, kutokana na msiba mzito wa vifo vya Watawa wanne, wa Shirika la Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu pamoja na dereva wao, waliofariki dunia katika ajali ya gari mkoani Mwanza.
Waliofariki dunia ni Mama Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu duniani, Katibu Mkuu wa Shirika hilo, Masista wawili pamoja na dereva wao, katika ajali baada ya gari walilokuwa wakisafiria, kugongana na gari jingine.
Watawa hao ni Sista Lilian Kapongo (raia wa Tanzania), Mama Mkuu wa Shirika hilo duniani, Sista Nerina De Simone (raia wa Italia), Katibu Mkuu wa Shirika hilo duniani, Sista Damaris Matheka (raia wa Kenya), Sista Stellamaris Muthini (raia wa Kenya), na dereva wao Boniphace Peter Msonola, mkazi wa Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, ametoa ufafanuzi na kukanusha kwamba si kweli kwamba Wakatoliki wanaabudu sanamu, bali wanamwabudu Bwana Yesu Kristo, aliyejinyenyekesha, akatii mpaka kufa msalabani.
Aliyasema hayo hivi karibuni, katika homilia yake wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu, ya Sikukuu ya Fumbo la Kutukuka kwa Msalaba, iliyofanyika katika kituo cha Hija – Pugu, jimboni humo.

VATICANCITY, Vatican

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Leo XIV, anatarajia kutembelea na kuzindua sehemu iliyoanzishwa kwa matakwa ya hayati Papa Fransisko, sanjari na kuadhimisha Liturujia ya Neno na Baraka ya kituo cha Borgo Laudato si.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mawasiliano ya Kituo cha Mafunzo ya Juu ya Laudato si, inaeleza kwamba ziara hiyo itafanyika Septemba 5 mwaka huu, na kwamba tukio hilo linatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni masaa ya Ulaya, ili kuzindua rasmi Borgo Laudato si, mahali ambapo kwa karne nyingi yamekuwa ni makazi ya Mapapa, ambayo sasa yamefunguliwa kwa umma, na ambapo kanuni zilizomo katika Waraka wa Kitume wa Laudato si’, mwaka huu zinaadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake.

VATICAN CITY, Vatican

Baba Mtakatifu Leo XIV, hivi karibuni amekutana na wahudumu wa altareni wapatao 360 kutoka Ufaransa, katika fursa ya hija yao jijini Roma, pamoja na Mapadri na Maaskofu wao kama sehemu ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya matumaini.
Katikati ya masuala ya kimataifa, pamoja na maumivu ya kibinafsi kutokana na hasara au wasiwasi, Papa aliwaalika vijana hao kumtazama Yesu ambaye ana uwezo wa kuwaokoa.

NAIROBI, Kenya

Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaraza ya Maaskofu Wanachama Afrika Mashariki (AMECEA), Padri Anthony Makunde wakati wa uzinduzi wa Sera ya Mawasiliano ya AMECEA, ameeleza kuwa waraka huo unaweza kutumika kama mwongozo wa mikutano mingine katika kanda hiyo, wakati wa kuandaa sera zao za mawasiliano.
Akiwahutubia washiriki mtandaoni na waliokuwepo  wakati wa uzinduzi, katika Madhabahu ya Consolata jijini Nairobi, Kenya, Padri Makunde alisema “Sera ya Mawasiliano ya Kijamii sio waraka wa ndani wa Sekretarieti tu, bali inakusudiwa kutumika kama marejeleo ya mikutano ya wanachama na dayosisi, wakati wanaunda sera zao za mawasiliano kitaifa na Jimbo.

NAIROBI, Kenya

Chama cha Wanachama wa Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (AMECEA), kimezindua Sera yake ya Mawasiliano na kuzindua Programu mpya ya redio ya kidijitali.
Afisa kutoka Kongamano la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar (SECAM), Charles Ayetan, amepongeza hatua hiyo akisema kwamba hatua hiyo muhimu sio tu kuhusu teknolojia, bali pia ni kuhusu kuimarisha ushirika, ushirikiano na utume wa Kanisa wa Uinjilishaji.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu amezindua Warsha kwa Waamini wote wa Jimbo hilo, inayotarajiwa kufanyika Novemba 29 mwaka huu, katika viwanja vya Parokia ya Kristo Mfalme - Tabata.
Uzinduzi huo aliufanya hivi karibuni Posta jijini Dar es Salaam, akiwasihi Waamini wote kujiandikisha na kushiriki kwa wingi katika Warsha hiyo, ambapo ndani yake kutakuwa na semina itakayohusisha mada mbalimbali.

Page 1 of 52