Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Na Mwandishi Wetu

Katika makala haya kuhusu Ubatizo wa Bwana, Mwadhama Protace Kardinali Rugambwa katika mahubiri yake, ametumia fursa hii kufafanua alama muhimu, zilizojionesha wakati Kristo Yesu alipobatizwa mtoni Yordani.

Anasema kwamba alama ya kwanza ni Maji: Alama ya kifo na uhai; Mbingu zikamfunukia, Roho Mtakatifu akashuka juu yake kama hua; Alama ya pili ni kufunguka kwa mbingu; Alama ya mabadiliko ya ndani ya mwanadamu, mbele ya Mwenyezi Mungu; Alama ya tatu ni Roho Mtakatifu aliyemshukia Kristo Yesu na sauti ya Baba wa milele ikasikika: Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu.

Ubatizo ni sakramenti inayotuingiza katika Ukristo, ni sakramenti inayotuondolea dhambi ya asili na adhabu zake zote. Ni kwa njia ya Ubatizo tunazaliwa upya kwa maji na Roho Mtakatifu, na hivyo tunakuwa ni watoto wa Mungu na wa Kanisa.

DAR ES SALAAM

Arone Mpanduka

Michel Kuka Mboladinga, ambaye pia anajulikana kama Michel Kuka, Michel Nkuka, au kwa jina la utani “Lumumba” na “Lumumba Vea”, ni shabiki wa soka wa timu ya taifa ya DR Congo, anayejulikana kwa tabia yake ya kipekee, wakati wa mechi za timu ya taifa ya kandanda ya DR Congo. 
Amekuwa shabiki kindakindaki wa taifa la Congo tangu mwaka 2013, ambapo amekuwa akisimama jukwaani bila kutikisika katika michezo yote. Amekuwa akiiga mkao wa sanamu ya mwanasiasa wa zamani na mkombozi wa taifa hilo, Patrice Lumumba mjini Kinshasa.
Jamaa huyu amejizolea umaarufu zaidi kwa vyombo vya habari vya kimataifa, wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika la 2025, nchini Morocco. 

London, Uingereza
Kiungo wa kati wa Tottenham, Rodrigo Bentancur, anahitaji upasuaji wa misuli ya paja, na anatarajiwa kukosa angalau miezi mitatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay, ambaye amekuwa mchezaji muhimu kwa timu ya Thomas Frank msimu huu, alipata jeraha hilo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Spurs dhidi ya Bournemouth wiki iliyopita.

London, Uingereza
Mshindi wa fainali wa zamani wa Wimbledon, Milos Raonic, alisema kwamba amekuwa mtu mwenye bahati zaidi kutimiza ndoto zake, alipotangaza kustaafu kutoka tenisi.
Mkanada huyo mwenye umri wa miaka 35, alimshinda Roger Federer na kufikia shindano la Wimbledon mwaka wa 2016, ambapo alishindwa moja kwa moja na Andy Murray wa Uingereza.
Raonic, ambaye alishinda mataji nane ya ngazi ya ziara, alifikia kiwango cha juu cha dunia cha tatu mwaka huo huo, baada ya pia kufika nusu fainali ya Australian Open.

DAR ES SALAAM

Na Nicolaus Kilowoko

Kocha Mkuu wa klabu ya soka ya Simba, raia wa Afrika Kusini Steven Barker, baada ya kuiongoza klabu hiyo kwenye michezo mitatu ya michuano ya Mapinduzi Cup 2026, ametoa maagizo kwa uongozi wa klabu hiyo, kusajili wachezaji wanne kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT), limeandaa mikakati ya kumleta bondia maarufu duniani, Manny Pacquiao, nchini Tanzania, kwa ajili ya mashindano ya semi Pro fights ya BFT.
Lengo la BFT kumleta Pacquiao nchini Tanzania, ni kwa ajili ya uzinduzi wa mashindano hayo, pia atashiriki matukio ya kijamii ya kuinua mchezo wa ngumi hapa nchini.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Klabu ya Singida Black Stars, imesema kuwa haina ukaribu wala urafiki wowote na klabu ya Yanga, hasa kwenye kupeana wachezaji na kupeana matokeo, kama watu wanavyodai.
Singida imeyasema hayo, wakati wimbi la kuuziana na kupeana wachezaji wa mkopo likishamiri, katika kila dirisha la usajili hapa nchini.
Katika dirisha dogo la sasa la usajili, Singida iliwatoa kwa mkopo wachezaji Mohammed Damaro na Marouf Tchakei kwenda Yanga, huku Yanga ikimtoa Mamadou Doumbia kwa mkopo kwenda Singida, jambo ambalo wadau wa soka wakalazimika kuweka hadharani shaka yao, kuhusiana na timu hizo mbili.

Na Dkt. Felician B. Kilahama

Namshukuru Mwenyezi Mungu aliye mwingi wa rehema, aliyeumba wanadamu kwa sura na mfano wake. Hili ni “wazo mbadala”, ikimaanisha kwamba kuna kinachotakiwa kufanyika, lakini katika harakati za utekelezaji likajitokeza ‘wazo mbadala’.
Uchaguzi Mkuu ulifanyika Oktoba 29, 2025, na aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, akatangazwa mshindi na kuapishwa rasmi Jumatatu, Novemba 3, 2025.
Baada ya zoezi hilo kukamilika, Rais aliunda Baraza la Mawaziri, ambalo pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Viongozi wakuu wa Halmashauri husika, kwa pamoja inakuwa Serikali inayoongozwa na Rais.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, kuna sehemu ambazo wananchi waliomba serikali itakayoundwa, kuanzisha wilaya na halmashauri mpya, ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma wanazohitaji, ikiwemo kutatuliwa kero haraka iwapo ofisi husika zitakuwa karibu.

NA PAUL MABUGA

Ilikuwa ni usiku wa vilio, hasira, lakini pia fahari kubwa. Jumapili iliyopita nchini Morocco, dunia ilishuhudia vijana wa Taifa Stars wakiondolewa kwenye michuano ya AFCON 2025, kichwa cha juu dhidi ya wenyeji Morocco.
Kufungwa goli 1-0 na timu namba moja barani Afrika, huku mwamuzi Boubou Traoré, akionekana kuwa “mchezaji wa 12” wa wapinzani, ni jambo ambalo halitafutika haraka kwenye akili za Watanzania.
Dakika ya mwisho ya mchezo itabaki kuwa jeraha, mchezaji wa Stars anaangushwa ndani ya kumi na nane, dunia nzima inaona ni penati ya wazi, lakini filimbi ya mwamuzi inabaki kimya, na VAR inajiziba macho.
Tulitolewa kama “ndama” anayepelekwa machinjioni, lakini kabla kisu hakijagusa shingo, ndama huyu alionesha kuwa ana pembe za chuma.
Hata hivyo, kuna mambo matano ya Stars kujivunia katika AFCON hii: Moja ikiwa ni kuvunjwa kwa mwiko wa miaka 45, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980, Tanzania imeweza kuvuka hatua ya makundi, na kuingia hatua ya mtoano (Round of 16).

NA REMIGIUS MMAVELE

Januari 12, 1966, katika Mji wa Matadi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alizaliwa mtoto ambaye alipewa jina Didier Masela Ndudi Bakisa Ntadilu, ambaye baadae alikuja kuwa maarufu katika sanaa ya muziki, akiendelea kutumia jina lake lile lile Didier Masela.
Ni baba wa watoto, yaani ana mke na watoto, hivyo yeye ni baba wa familia. Didier ni mwanzilishi wa kundi la Wenge Musica, ambaye anasema wazi kuwa hakuzaliwa jijini Kinshasa, akitamba kwamba haoni aibu yeyote kutamka hadharani, kuwa amezaliwa kijijini.
Kitendo cha kuwa muasisi wa kundi la Wenge Musica, hakijamfanya athaminike kama mwanzilishi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, licha ya kwamba ni kweli wazo la kuundwa kundi la Wenge Musica alilitoa yeye, Didier anafikiri kutokana na wazo lake hilo, amewasaidia watu walio wengi. Anaamini kwamba, wako wengi ambao walikuwa hata hawajitambui kama wao ni wasanii, alikuwa akiwahimiza, kuwashurutisha na kuwasukuma. 
Didier anasema kwamba, ubunifu wa wazo hutokana kwanza na mtu mmoja na wala sio wawili, wazo hilo linaweza likakubalika na watu wengine. Kwa maana hiyo, wazo la kuanzisha kundi la Wenge Musica, lilitokana na yeye Didier, tena ni yeye ambaye aliwaita kila mmoja kati ya watu ambao anawafahamu. Watu kama Alain Prince Makaba, Werrason na Jb Mpiana, aliwaleta yeye katika kundi la Wenge Musica.