Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

NAIROBI, Kenya

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka Taasisi 26 za Elimu ya Juu nchini Kenya, wamepewa ujuzi unaojumuisha ubora wa kiakili na huduma ya kujitolea, ili kufikia uongozi wenye mabadiliko na athari kubwa kwa jamii.
Programu ya Uongozi ya Kizazi Kijacho (NGLP), ambayo hapo awali ilikuwa Programu ya Udhamini wa Kikatoliki, ambayo inazingatia mafunzo ya kitaaluma na uongozi kwa wanawake, wanaume, na Waamini wa kidini wa Kiafrika, inawafunza wasomi wake kuwa Miale ya Matumaini, ambapo imeitwa Kutumikia, Kubadilisha, na Kuhamasisha.
Katika tafakari iliyotolewa na Padri John Webootsa, mwanachama wa Comboni Missionaries of the Heart of Jesus (MCCJ), kwa zaidi ya wanafunzi 150 wakati wa kumbukumbu zao katika Bustani ya Ufufuo, katika Mji Mkuu Nairobi, Kenya, alisema kuwa jamii kwa sasa ina njaa ya uongozi halisi na uwazi wa maadili.

VATICAN CITY, Vatican

Katibu Mkuu wa Vatican, Mwadhama Pietro Kardinali Parolin, ametaka ushiriki wa Marekani na jukumu kubwa kwa Ulaya, katika juhudi za kukomesha mzozo wa Ukraine, akisisitiza kwamba China pia ina neno la kusema kwa ajili ya amani.
Aliyasema hayo hivi karibuni, aliposhiriki katika Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù, akiashiria kumbukumbu ya miaka 40 ya kutambuliwa kwake, kama Taasisi ya Kisayansi ya Kulazwa Hospitalini na Matibabu.
Akizungumzia mkutano na Waziri Mkuu wa Hungaria, Viktor Orbán, aliuelezea kama majadiliano mazuri, na kwamba wanajaribu kuleta misimamo yao karibu zaidi.

DAR ES SALAAM

Na Shemasi George Timalias

Karibu ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, katika tafakari hii, inayotugusa kwa karibu sana, ambayo inakumbusha Sikukuu ya Watakatifu wote, kila ifikapo tarehe Mosi Novemba ya kila mwaka, lakini pamoja na Watakatifu, kuna ndugu zetu Marehemu wote waliotutangulia mbele ya haki, ambapo Mama Kanisa anatupatia fursa ya kuwakumbuka, kila ifikapo  tarehe 2 ya mwezi Novemba na kuendelea hadi mwisho wa mwezi.
Kwa hiyo tuanze tafakari hii, sehemu ya kwanza ya Watakatifu. Fundisho kuu tunalopata katika siku hii ya watakatifu wote, ni msisitizo wa maisha yetu kuishia mikononi mwa Mungu aliyetuumba huko mbinguni.

Katika safu hii ya Chimba Chimba Historia ya Kanisa wiki iliyopita, tuliendelea kuwaletea historia ya kuibuka kwa Dola ya Kikristo, hususani tuliwajuza kuhusu Faida na Hasara za Dola ya Kikristo. Leo tunawaletea historia ya Miundombinu ya Kanisa kuanzia Karne ya nne na tano. Sasa endelea…

Watumishi wa Kanisa na Mitaguso:
Bwana wetu Yesu Kristo, aliacha amewachagua na kuwaweka mitume 12 na wafuasi 70 (72), ili waendeleze kazi aliyoianza (Lk. 6:13-16; 10:1-12). Hawa walirithiwa kama Maaskofu na Mapadri.
Katika Kanisa la mwanzo, polepole kufuatana na mahitaji katika misingi aliyoiweka Kristo, miundombinu hiyo iliongezeka na kuboreshwa.
Kuanzia Karne ya nne na tano, palikuwepo na madaraja saba katika watumishi wa Kanisa. Kati ya madaraja hayo, madogo ni manne yakiwemo Mfungua Mlango, Msomaji, Mtoa Mashetani na Mtumishi wa Ibada, na madaraja makubwa ni matatu, Ushemasi, Upadri na Uaskofu.

Padri Andreas Chitanda Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Malkia-Luagala Jimbo Katoliki la Mtwara, akibariki kinanda kipya cha Kigango cha Kutukuka kwa Msalaba-Lyenje jimboni humo, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika iliyoadhimishwa hivi karibuni.

Waimarishwa wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara wa Parokia ya Mtakatifu Toma – Muungano, Jimbo Katoliki la Bagamoyo, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo, iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mkuu-Mtume, Mabwepande jimboni humo. Wa tatu kulia ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Thomas Mtei na kushoto ni Paroko Msaidizi, Padri Dickson Sambala.

Moshi

Na Paul Charles Mabuga

Wiki moja tu inatosha kunasa moyo wako, katika mtego mtamu wa pilikapilika za Moshi. Huu si mji wa kawaida, bali ni lulu iliyolala katika kivuli kitukufu cha Mlima Kilimanjaro.
Huku ukiahidi utulivu wa kitalii, uhalisia wake umejaa mizunguko ya kusisimua, milio isiyotarajiwa, na siri za kitabibu zinazofichwa kwenye glasi ya maziwa ya ngamia, na kikombe cha kahawa bora kabisa duniani.
Nilipowasili, hali ya hewa ilinikumbatia kwa ubaridi laini wa majira haya, ule unaochochea hamu ya kahawa ya moto hata mchana. Lakini ghafla, palikuwa na mabadiliko ya joto! Joto jipya lilianza kuhisiwa ghafla, kana kwamba Mlima Kilimanjaro ulikuwa umeamua kuachia pumzi yake ya joto badala ya baridi. Mabadiliko haya ya ghafla yananukia mabadiliko ya tabianchi, yanayobadilisha mood ya mji.

Na Arone Mpanduka

Mchezo wa kuchapana fimbo ni aina ya mchezo wa jadi, unaopatikana katika tamaduni nyingi za Kiafrika, ikiwemo Afrika Mashariki hasa Somalia (Istunka), Ethiopia, Sudan, na hata baadhi ya jamii nchini Kenya na Tanzania.
Hapa chini nitakuelezea kwa mtazamo wa jumla wa Kiafrika, kisha nitagusia toleo la Kisomali (Istunka), na toleo la Waswahili au Wamasai kwa ulinganisho wake.
Mchezo huu hauna jina moja pekee, bali una majina mbalimbali hasa katika mataifa kadhaa barani Afrika.

Miami, Marekani
Pambano la maonyesho la Jake Paul dhidi ya Bingwa wa Dunia wa uzani wa lightweight Gervonta Davis limeahirishwa.
Pambano hilo, lililopangwa kufanyika Novemba 14 mwaka huu huko Miami, lilipangwa kutikisa vichwa vya habari duniani kupitia Netflix.
Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya kesi kufunguliwa dhidi ya Davis na mpenzi wake wa zamani akimshtaki kwa unyanyasaji wa kijinsia, utekaji nyara na kuumiza hisia kwa kukusudia.