Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), kinalaani vurugu, mauaji na uharibifu wa mali, vilivyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Chama hicho pia kimetoa pole kwa wote waliopoteza ndugu au mali, na kuunga mkono  agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, la kufanya uchunguzi wa kina, na kuwawajibisha wahusika wote kwa mujibu wa sheria.

Dar Es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Katika kuadhimisha Wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imezindua rasmi kitengo kipya cha kusafisha damu (dialysis unit), kwa wagonjwa wa moyo wanaopata matatizo ya figo, hatua inayolenga kuboresha huduma za tiba jumuishi kwa wagonjwa hao.
Kitengo hicho chenye mashine za kisasa, zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200, kimeanza kutoa huduma mara moja baada ya kuzinduliwa, kikiwa na uwezo wa kusafisha damu kwa zaidi ya wagonjwa nane kwa siku.

Mbeya

Na Mwandishi wetu

Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ya Kanisa Katoliki nchini, wameadhimisha Misa Takatifu za kuwaombea watu waliouawa na kujeruhiwa, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu, huku wakitoa kauli tofauti tofauti na kukemea, kuhusu hali ya uvunjifu wa amani iliyotokea wakati wa uchaguzi huo.

Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap, amesema kuwa hakuna amani bila haki, kwani haki ni msingi wa lazima wa amani.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema hayo katika Adhimisho la Misa Takatifu, ya Kuwaombea watu waliouawa katika wiki ya Uchaguzi Mkuu Tanzania, iliyoadhimishwa hivi karibuni, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo.

Dar es Salaam

Na Laura Mwakalunde

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amewaonya Waamini kutoruhusu wao kuwa karakana ya shetani.
Alisema hayo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya uzinduzi wa nyumba ya Mapadri, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Consolatha-Mbezi Makabe.
“Kila Mkristo inampasa kuwa na maamuzi kwa kuachana na mambo ya kale, aibu ya giza, kwani inasikitisha kuona Mkristo anakwambia bado kidogo,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aidha, aliwataka Waamini watambue kuwa wao ni warumi wa leo, kwa sababu Mtume Paulo huwa anafundisha ukweli wa mambo ya kale, ya aibu na ya giza, kwa kutoruhusu akili na utashi wao kuwa kichaka cha dhambi.

Same

Na Mathayo Kijazi

Kutokana na kuwepo kwa matukio ya ajali za barabarani za mara kwa mara, Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogath Kimario, ameandaa mkakati wa kujenga Groto ya Bikira Maria Mwombezi wa Wasafiri, kando ya barabara katika eneo la Maligo jimboni humo, ili kusaidia kuzuia ajali hizo.
Askofu Kimario aliyasema hayo hivi karibuni, ambapo alibainisha kuwa eneo hilo mara nyingi hutumiwa na wasafiri, kama sehemu ya huduma za maliwato, hivyo ni vema kujenga Groto hiyo ili wasafiri wapate huduma za kiroho, ikiwemo kuombea safari zao.
Aliongeza kuwa wanafanya hivyo ikiwa pia ni sehemu ya maandalizi, kuelekea katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50, tangu Same ilipotangazwa kuwa Jimbo Katoliki, ambayo kilele chake ni Februari 3, 2027, hivyo katika kamati yao ya maandalizi, wameona ni vema kujenga Groto hiyo ya Bikira Maria Mwombezi wa Wasafiri.

Morogoro

Na Angela Kibwana

Mhashamu Askofu Lazarus Msimbe- SDS, wa Jimbo Katoliki Morogoro, amesema kuwa sheria ni kwa ajili ya watu na sio watu kwa ajili ya sheria, kwa sababu watu ni muhimu zaidi kuliko taratibu na sheria, kwani sheria isiyomsaidia mtu haina maana.
Askofu Msimbe alisema hayo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu, katika mahafali ya  wahitimu wa 14 wa Chuo cha Katekesi, ambapo kati yao wahitimu tisa ni kutoka Chuo cha Mtakatifu Karoli Lwanga-Mzumbe, na  watano kutoka Chuo cha Katekesi  cha Mtakatifu Yoseph Mfanyakazi Bigwa, iliyofanyika katika Chuo cha Katekesi Mzumbe jimboni Morogoro.
Askofu Msimbe kadiri ya tafakari ya Injili husika, alieleza kuwa huduma kwa watu ndio hitaji namba moja, kwa sababu dai la kwanza kwa yeyote ni dai la mahitaji ya binadamu, kwa kuwa sheria ambayo haimsaidii mtu haina maana.

Kagera

Na Silivia Amandius

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wakili Amon Mpanju, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani Kagera, kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wengine, ili kuwaleta wananchi pamoja.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Mkoa wa Kagera, Mpanju alisema kuwa maendeleo ya kweli yapo kwa wananchi, hivyo ni muhimu watumishi hao kuwafikia hadi ngazi za vijiji.

NJOMBE

Na Mwandishi wetu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. John Jingu, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani Njombe, kutunza na kutumia kwa umakini pikipiki walizopewa na serikali, ili kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Dk. Jingu alisema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki nane, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa ngazi ya Kata, mkoani humo.

Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kwamba huduma ya mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) katika barabara ya Morogoro kuelekea Kimara, Moroco na Barabara ya Kilwa kutoka katikati ya mji kwenda Mbagala imesitishwa kwa muda.
Hatua hiyo imetokana na kuaharibika kwa miundombinu ya barabara hizo.
Chalamaila (pichani) alitoa tamko hilo jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa Habari na kutaja kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua ya kufanya tathmini ya hasara iliyopatikana na kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo, hivyo pindi itakapokaa sawa huduma hiyo itarejea.
“Tumelazimika kusitisha huduma ya usafiri huo kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa uchaguzi na kundi la waandamanaji na kusababisha kuharibika kwa mifumo yote ya ukatajai tiketi na sehemu za kupakilia abiria hivyo sasa tunatoa maelekezo kwa LATRA kutoa vibali vya muda kwa wamiliki wa daladala hili waweze kuwahudumia wakazi wa maeneo hayo ambao kwa sasa wanahitaji kufika mjini,”alisema Chalamila.