Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waamini waaswa kutopokea Ekaristi Takatifu kimazoea

Waamini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa katika maandamano ya Ekaristi Takatifu baada ya adhimisho la Misa Takatifu ikiwa kama ishara ya kumtangaza Yesu wa Ekaristi kwa jamii nzima. Waamini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa katika maandamano ya Ekaristi Takatifu baada ya adhimisho la Misa Takatifu ikiwa kama ishara ya kumtangaza Yesu wa Ekaristi kwa jamii nzima.

Na Waandishi Wetu

Waamini wameaswa kutopokea Ekaristi Takatifu kimazoea huku wakia hawana maandalizi mazuri kiroho.
Ujumbe huo umetolewa na maaskofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Mhashamu Sana Jude Thaddeus Ruwa’ichi na Askofu Msaidizi Mhashamu Henry Mchamungu kwa nyakati tofauti wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu ya Sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana Wetu Yesu Kristo
Akiwa katika Kanisa Kuu la Mt. Yosefu, Mhashamu Sana Jude Thaddeus Ruwa’ichi alisema waamini wanapaswa kukumbuka kuwa Ekaristi Takatifu si kitu cha kupokelwa kimazoea bali kinahitaji tafakari na maandalizi ya kiroho.
“Mnatakiwa kutambua kuwa Ekaristi siyo kitu cha mazoea wala cha kubahatisha bali ni adhimisho Takatifu sana na kuu la wokovu wetu,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Aidha alisema kuwa kila mtu anatakiwa kufahamu ni nini anafanya pale kwenye adhimisho la Misa Takatifu kwa sababu ndipo kwenye kiini cha imani.
Mbali na hayo aliwasisitiza waamini kuziishi Sakramenti kwa imani, upendo na ibada kwa ajili ya kupata uzima wa kimungu.
 Alisema kwamba wana wa Israeli walipokuwa jangwani walimlalamikia Musa kwa kuwa na njaa na kusema ni bora angewaacha utumwani kuliko kuwapeleka jangwani jambo ambalo alisema lilionesha jinsi binadamu walivyo vigeugeu.
Askofu Ruwa’ichi aliwataka waamini wafahamu kwamba utumwa ni mateso japo kuwa wanadamu wengi ni vigeugeu wanaoweza kutakani kurudi utumwani wanapopata shida katika safari ya ukombozi.
Askofu Ruwa’ichi aliwataka waamini watambue kuwa wao ni Taifa jipya la Mungu na wako hivyo kwa sababu ya sadaka ya Yesu Kristu ya kukubali kujishusha na kutwaa ubinadamu na kufa kifo cha aibu.
Sambamba na hayo alisema kuwa Yesu Kristu alikubali kuteswa na kufa msalabani kwa ajili ya kutaka kukomboa ulimwengu kutoka katika dhambi na kabla ya kufa kwake aliweka Ekaristi Takatifu ikiwa alama ya upendo wake mkuu kwa wanadamu.
Pia alisema kuwa Ekaristi ni ukumbusho wa mateso,kifo  na ufufuko wa Yesu Kristu kwani katika Ekaristi kila mtu amepewa sadaka ya ukombozi yenye kuwapatanisha watu na Mungu.
Askofu Ruwa’ichi aliendelea kusema kuwa Ekaristi ni Sakramenti Kuu ya wokovu ambayo Yesu Kristu aliitoa kama zawadi kwa mitume wake kwa ajili ya kuiadhimisha na kupokea mwili na damu ya Yesu Kristu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.