Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

KASESE, Uganda

Padri Raphael Balinandi Kambale ameadhimisha Jubilei ya Dhahabu katika Parokia ya Nsenyi, Jimbo Katoliki la Kasese nchini Uganda, akiwasihi Mapadri vijana na Wakristo kwa ujumla, kujenga upendo kwa Kanisa, na kujitolea kwa ajili ya Miito.
Padri Balinandi, ambaye kwa sasa ni Padri mzee zaidi katika Jimbo Katoliki la Kasese, alipewa Daraja Takatifu la Upadri, Desemba 14 mwaka 1974 katika Parokia ya Nsenyi na Askofu Vincent J. McCauley, mbele ya Askofu Sarapio Magambo na Askofu Kathaliko Emmanuel, kutoka Jimbo Katoliki la Butembo-Beni.
Yeye alikuwa Padri wa tatu kutoka Jimbo Katoliki la Kasese, akifuatiwa na Monsinyori Augustine Muhindo Hayati, aliyepewa Daraja la Upadri wa kwanza mwaka 1958 na Padri Louis Isingoma Byakuyamba mwaka 1972.
Katika hotuba yake muda mfupi baada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kasese, Mhashamu Francis Aquirinus Kibira Kambale, Padri Balinandi alitajwa kuwa mtu wa thamani katika Jimbo na Wilaya kwa ujumla, ambaye amechangia maendeleo ya kiroho, kitamaduni na mazingira.
Askofu Francis Kibira alisema kuwa Ndoa Takatifu inachukuliwa kuwa ni Sakramenti yenye nguvu katika Kanisa Katoliki ambayo wanandoa wanapaswa kuilinda kwa wivu kwa sababu ni mfugaji wa Sakramenti nyingine.
Vile vile, Askofu Kibira ambaye alitoa wito wa mafunzo ya Katekesi miongoni mwa watoto, alisema kwamba ili Kanisa liwe na Mapadri wazuri na wanandoa miongoni mwa Miito mingine kanisani, wazazi wanatakiwa kuwa na sababu na kuweka thamani katika ndoa ili kuwalea watumishi makini wa Kanisa na Jumuiya.
Katika ujumbe wake, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Gulu, Mhashamu John Baptist Odama, mwanafunzi mwenza wa Padri Balinandi, alirejea maelezo ya watu wengine kuhusu Padri, kwamba yeye ni mtu mwenye imani kubwa kuhusu maisha kama Kasisi.
Mbali na hilo, aliendelea kwa kusema, “Nina kumbukumbu zake za kuwa na shauku kubwa ya liturujia, na kutamani sana kufuata kanuni za kiliturujia na Neno la Mungu.”
Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Kasese, Mhashamu Egidio Nkaijanabwo alisema kuwa Padri Balinandi alikuwa mtu wa mila nzuri, na alipenda utamaduni wake.
Kupitia utamaduni wake, kujifundisha, na kupitia elimu yake zaidi, Padri Balinandi ameonekana kuwa na ujuzi katika lugha ya Lhukonzo.
Miongoni mwa umahiri mwingine, alitafsiri vitabu vingi vya kiliturujia katika lugha ya kienyeji, zaidi ya yote aliyoheshimu Ufalme wake.
Katika mahubiri yake, Padri Expedito Masereka, Msimamizi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bukangara, aliwataka Wakristo kujifunza kutoka kwa Padri Balinandi kujiendeleza kiujumla kwa kuanza na wao wenyewe.
Mratibu huyo wa zamani wa Kichungaji, alimpongeza mshereheshaji huyo kwa michango yake ya umoja, na kukuza lugha ya Lhukonzo, kazi inayowalazimu Wakristo katika Miito mingine kutimiza wajibu wao kwa umakini na matumaini, kama inavyotarajiwa hadi mwisho.
Mjubilei huyo, Padri Balinandi Kambale akiwa na furaha tele, alimpongeza Askofu Kibira kwa upendo na matunzo katika uzee wake, akisema kuwa aligubikwa na upendo, ukarimu na uangalizi alioonyeshwa na Wakristo, na watu wema.
Naye Mkuu wa Walei wa Jimbo Katoliki la Kasese, George Mayinja, aliwataka wazazi kuwalea watoto wao kulingana na huduma ya Kanisa, lakini pia kuwekeza katika Elimu yao.

LUSAKA, Zambia
Kituo cha televisheni cha Kikatoliki nchini Zambia, Lumen TV-Z kimepata msukumo mkubwa kwa kuweka mfumo wa umeme wa jua wa KVA 11 wenye thamani ya Kwacha 270,000 ambayo ni takriban dola 9,815, sawa na Shillingi 23,485,910.45/- za Kitanzania.
Mfumo wa jua uliotolewa na GEI Power Limited na kukabidhiwa rasmi hivi karibuni katika kituo hicho, unashughulikia changamoto zinazoendelea nchini za uondoaji wa shehena, na ulitolewa kama sehemu ya ahadi iliyotolewa na GEI wakati wa chakula cha mchana cha Lumen TV mnamo Septemba, ikionyesha ushirikiano unaoendelea kati ya mashirika hayo mawili.

VATICAN

Baba Mtakatifu Fransisko amewataka Waamni kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo, akiwasisitiza kupokea zawadi ya uhai kwa moyo wa upendo, shukrani na ukarimu.
Aliyasema hayo wakati wa Dominika ya Nne ya Majilio, Mwaka ‘C’ wa Kanisa, ambapo pamoja na mambo mengine, Baba Mtakatifu alisema, “Bikira Maria ambaye baada ya kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu, anakwenda kwa haraka kumtembelea binamu yake Elizabeti, ambaye katika uzee wake, alikuwa ni mjamzito.”
Aidha, aliwaalika Waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai tangu pale mtoto anapotungwa mimba, hadi mauti ya kawaida yanapomfika, kadri ya mpango wa Mungu.
Sambamba na hayo, Baba Mtakatifu anakaza kusema kwamba Kanisa linataka kujitosa kuwahudumia kwa ukarimu na upendo watoto wadogo ambao bado hawajazaliwa zaidi ya wengine wote, kwani hao ni watu wasio na ulinzi wala hatia.
“Wanawake hawa walikuwa na kila sababu ya kufurahia kutokana na miujiza iliyotendwa ndani mwao, mwaliko ni tafakari ya kina kuhusu uwepo wa Mungu kati ya waja wake na kwamba, huruma na upendo wake unamwandama mwanadamu kwa njia ya zawadi ya maisha, kwa kila mtoto anayebebwa tumboni mwa mama yake, kama ilivyo kwa wanawake wengi na kati yao kuna wale ambao wanatazamia kwa imani na matumaini, kuzaliwa kwa watoto wao,” alisema Baba Mtakatifu.
Vile vile, aliwaalika Waamini kupokea zawadi ya uhai kwa moyo wa upendo, shukrani na ukarimu, akisema, “Hata watoto ambao hawajazaliwa, wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Jamii isipojifunza kuwalinda na kuwatunza watu dhaifu, sheria ya mwenye nguvu mpishe, itatawala Dunia. Maskini wanao upendeleo wa pekee mbele ya Mwenyezi Mungu. Wao ni walengwa wa kwanza wa Habari Njema ya Wokovu, ni amana na utajiri wa Kanisa. Wao ni dira na ufunguo wa kuingilia mbinguni.”
Alisema pia kuwa inasikitisha kuona kwamba katika baadhi ya Nchi, utamaduni wa kifo unalindwa kisheria, jambo linalokwenda kinyume cha haki msingi za binadamu, utu na heshima yake.
Aliongeza kwamba maisha ya binadamu ni Matakatifu, hivyo yanapaswa kulindwa na kuendelezwa, akisema kuwa utoaji mimba si kitendo cha maendeleo, bali ni ukiukwaji wa haki msingi za binadamu.
Pia, alibainisha kwamba Kanisa linapenda kuwasaidia wanawake kutekeleza vyema dhamana na wajibu wao wa kulea na kutunza vyema watoto, ambao ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu.
Alisema kuwa katika kipindi hiki cha Sherehe za Noeli ambapo sehemu mbalimbali zinapambwa kwa taa na muziki wa Noeli, Waamini na watu wote wenye mapenzi mema, wanapaswa kuonesha furaha pale wanapokutana na wanawake wajawazito, au wale wanaowabeba watoto wao, tayari kumwimbia Mungu utenzi wa sifa na shukrani, kama ilivyokuwa kwa Elizabeti, akisema “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na mzao wa tumbo lako amebarikiwa.”
Alisisitiza kwamba hii inatakiwa iwe ni fursa ya kushukuru na kuwabariki watoto wote wanaozaliwa sehemu mbalimbali duniani.

VATICAN CITY

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Taleb Al Abdulmohsen, mwenye umri wa miaka 50, Daktari wa Afya ya Akili, aliyeingia nchini Ujerumani kunako mwaka 2006, hivi karibuni amevamia Soko la Noeli, lililoko mjini Magdeburg, nchini Ujerumani, na kusababisha vifo vya watu watano, na kujeruhi watu zaidi ya 200, na kati yao, watu 41 wako katika hali mbaya.
Kufuatia tukio hilo, Baba Mtakatifu Fransisko amesikitishwa na shambulizi hilo la kinyama, huku akionesha uwepo wake wa karibu kwa waathirika.
Alisema kwamba kwa masikitiko makubwa, anaungana na watu wenye mapenzi mema kuwaombolezea wale wote waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo, na kwamba, yuko karibu na wote walioguswa na kutikiswa na msiba kutokana na tukio hilo.
Aidha, Baba Mtakatifu Fransisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, aliwapongeza wale wote wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa shambulio hilo.
Papa anasali pia na kuwaweka waathirika wote chini ya Kristo Yesu, tumaini la waja wake, nuru inayoangaza kwenye giza la uvuli wa mauti, akiwaombea kwa moyo wote msaada na faraja kutoka mbinguni.
Mji wa Magdeburg ni maarufu sana kwa viwanda na bandari, na upo katikati ya Ujerumani kwenye ukingo wa Mto Elbe, ambapo wachunguzi wa mambo wanasema Taleb Al Abdulmohsen amevamia Soko la Noeli kwa kutoridhishwa na jinsi ambavyo Serikali ya Ujerumani inavyowatendea wakimbizi na wahamiaji, ila yeye bado anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa uchunguzi zaidi.

DODOMA

Na Angela Kibwana

Watu wenye ulemavu sawa na makundi mengine katika jamii, wana haki ya kunufaika na upatikanaji  wa haki ya Afya  ya Uzazi, kama haki ya msingi ya binadamu bila vikwazo, unyanyapaa  na ubaguzi wa aina yoyote.
Haki ya Afya ya Uzazi kwa watu wenye ulemavu imetamkwa na kuelekezwa kwenye Sera, Miongozo na Sheria mbalimbali za Kimataifa, Kikanda na Kitaifa kama vile: Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (2006), kifungu cha 25 (Article 25), umesisitiza watu wenye ulemavu, wana haki ya kupata huduma za afya bila ubaguzi
Sheria ya Tanzania kwa Watu Wenye Ulemavu (2010) kifungu cha 26, Kifungu kidogo cha Kwanza hadi cha tatu limesisitiza kuhusu haki ya kupata huduma ya afya na utengamao kwa watu wenye ulemavu, bila ubaguzi,Sera ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2004, imetambua suala la ulemavu kama haki za msingi za  binadamu.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, imeeleza watu wenye ulemavu ni wale wote wenye changamoto za muda mrefu za kimaumbile, kiakili na katika mfumo wa fahamu (intellectual or sensory), hivyo kukosa na kushindwa kushiriki sawa na makundi mengine ya kijamii katika kuzifikia fursa mbalimbali.
Takribani asilimia 11 ya watu kuanzia umri wa miaka saba (7) na kuendelea, wanaishi na ulemavu wa aina fulani, ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 9.3 (Sensa Mwaka 2012).
Hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu wenye ulemavu inatofautiana kati ya kijijini kwa asilimia 11.5 na mjini asilimia 10.6.
Mkoa wa Dodoma una idadi ya watu 299,689, sawa na asilimia 12.3 zaidi ya kiwango cha kitaifa cha asilimia 11, ukiwa ni mkoa wa sita kwa idadi kubwa ya watu wenye ulemavu (Sensa Mwaka 2022) nchini.
Pamoja na jitahada zote zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika na serikali, asasi zisizo za kiserikali na wadau wa maendeleo, kundi la watu wenye ulemavu, wameendelea kukabiliwa na changamoto nyingi za afya ya uzazi, zikijumuisha changamoto za kimazingira na kisera zinazo athiri upatikanaji na ufikikaji wa huduma za Afya, kwa mfano miundo mbinu isiyo rafiki, umbali na gharama za huduma na kukosekana kwa teknolojia saidizi.
Pia, unyanyapaa na mtazamo hasi kutoka kwa wana familia, jamii na watoa huduma za afya dhidi ya  haki ya huduma za Afya ya Uzazi kwa watu wenye ulemavu; Ujumuishaji hafifu wa watu wenye ulemavu kwenye programu na mipango mbalimbali ya afya; watoa huduma za afya kutokuwa na uelewa kuhusu masuala yanayohusu mahitaji ya watu wenye ulemavu, kama vile lugha ya alama, pamoja na namna ya kutoa huduma rafiki kwao; matumizi hafifu, pamoja na kutokuwa na takwimu sahihi za watu wenye ulemavu ili kujumuishwa kwenye mipango, bajeti na huduma za afya katika ngazi ya halmashauri, vituo vya kutolea huduma za afya, na jamii kwa ujumla.
Changamoto hizo zimeongeza uhatarishi zaidi kwa makundi ya wanawake na vijanawenye ulemavu, hali ikiwa mbaya  zaidi kwa wale wanaoishi vijijini wakikabiliwa na umaskini uliokithiri, pamoja na  ukatili wa kingono, kama vile Ubakaji na ndoa za kulazimishwa.
Kwa kutambua changamoto na umuhimu wa haki ya hudumu za Afya ya uzazi kwa watu wenye ulemavu kama ilivyoainishwa katika Sera, Miongozo na Sheria za Kimataifa, Kikanda na Kitaifa; Shirika la Marie Stopes Tanzania, kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Watanzania chini, ya ufadhili wa Marie Stopes International (MSI) kupitia mradi wa Investiment Fund (IF), wameligeukia kundi hili ambalo halijafikiwa ipasavyo  kwa kuwekeza fedha, utaalam na miundombinu, ili kutengeneza mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu kuzifikia huduma bora za Afya ya Uzazi.
Hayo ni kama vile, Uzazi wa Mpango, Huduma wakati wa Ujauazito, Kujifungua, baada ya kujifungua, Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto, elimu na taarifa sahihi kuhusu  Afya ya Uzazi na Ujinsia, pamoja na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika masuala yanayo athiri maisha yao, ikiwepo Afya Uzazi na Ujinsia kama ilivyoelezwa na Ndugu Goryo Moris Kitege, mtoa huduma za afya ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania
Pia, Ndugu Goryo alisema kuwa Shirika la Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na Serikali, wanaendelea kuona namna watakavyowajengea uwezo watoa huduma za afya namna kuwahudumia watu wenye ulemavu, pamoja na kufanya ulaghabishi (advocacy), kuhusu uboreshaji wa mazingira wezeshi ili kufikia kundi kubwa la watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali nchini.
Kwa mujibu wa  Ndugu  Amina Issa anayeishi na ulemavu wa kusikia kutoka Chama cha Viziwi Dodoma, anasema,  “Mara nyingi hatupati huduma stahiki kutoka kwa watoa huduma za afya kwa kuwa watoa huduma  hawajui Lugha ya Alama”
Pia, Amina anatoa mfano wa unyanyapaa wanaokutana nao watu wenye ulemavu, akisema, “Kuna wakati unakutana na kauli za kudhalilisha, kama vile ‘Hata wewe mtu mwenye ulemavu umeweza kupata ujauzito?’ Kauli hizi zina tuumiza sana,” kwani na sisi tunahisia na tuna haki ya kuwa na familia, pamoja na kufurahia maisha ya mahusiano na ujinsia kama watu wengine” hali hii inakatisha tamaa kwenda kupata huduma.
Vile vile katika kuendeleza jitahada za kuwafikia watu wenye ulemavu katika masuala ya Afya Uzazi; Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), wameendelea kutoa elimu na huduma bora za Afya ya Uzazi ambapo watu zaidi ya 300 wenye ulemavuwamepatiwa huduma na elimu kuhusu afya ya uzazi.
Justus Ngwantalima, Katibu wa SHIVYAWATA, anasisitiza kwamba ni muhimu kwa jamii kuwa na mtazamo chanya dhidi ya watu wenye ulemavu, ili kufanikisha lengo la usawa katika jamii kwa mujibu wa sera na sheria za nchi.
Kwa mujibu wa Omary Lubuva,  Mwenyekiti wa SHIVYAWATA  Dodoma,kuna haja ya kuboresha mfumo wa mawasiliano ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora  kwa watu wenye ulemavu.
Pia, wataalamu wa afya wanapaswa kupewa mafunzo maalum ya kushughulikia mahitaji ya kundi hili.
Aidha, watu wenye ulemavu wanapaswa kushirikishwa katika kupanga, kutekeleza na kutathmini mipango na bajeti za afya kama ilivyoelekezwa kwenye sera na miongozo mbalimbali ya kimataifa, na ya nchi kwa ujumla.
Hata hivyo, aliwashukuru Marie Stopes Tanzania pamoja na serikali kwa jitahada zao katika kuwashirikisha kushughulikia mahitaji yao; kwani si jambo jepesi kulifikia kundi kubwa kama hili la watu wenye mahitaji maalumu kwa wakati mmoja, hivyo nguvu ielekezwe  pia  kwa watu wenye ulemavu  walio vijijini kwa njia shirikishi na  endelevu.
Katika mahojiano ya mwandishi wetu na Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wilaya ya Bahi, Ndugu Agnes Mwabungulu, anasema kuwa vituo vingi vya afya havina miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.
Pia, anabainisha ukosefu wa wataalamu wenye ujuzi wa Lugha ya Alama kama changamoto kubwa.
Hata hivyo, amesema kuwa serikali kwa kutumia rasilimali chache zilizopo, pamoja na kupitia ushirikiano na wadau, wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali zinazo athiri utoaji, upatikanaji na utumiaji wa huduma za afya uzazi kwa watu wenye ulemavu, kulingana na sera na miongozo ya nchi.
Aliongeza kwa kusema  kuwa jitahada za kuwafikia watu wenye ulemavu, hazilengi tu kuwafikia katika hali yao ya uhitaji, bali kuzuia ulemavu kwa watoto wanaowazaa, unaoweza kuchangiwa na kukosekana kwa huduma bora kabla, wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua. Hivyo kuongeza changamoto zaidi kwao, serikali, jamii na watoto watakaozaliwa na ulemavu wa aina mbalimbali.
Mwisho, amewashukuru Marie  Stopes Tanzania na wadau wa maendeleo kwa ushirikiano wa, na kazi nzuri wanayoifanya katika Halmashauri ya Bahi, ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya ya Uzazi kwa mtoto na vijana.
Pia, wanawakaribisha kwa ushirikiano zaidi pamoja na wadau wengine, ili kuwakufikia watu wenye ulemavu, pamoja na makundi mengine yenye changamoto katika jamii.

DAR ES SALAAM

Na Remigius Mmavele

Daniel Zitani Ya Ntesa, maarufu kama Ntesa Dalienst, alikuwa mwimbaji\mtunzi wa Kongo ambaye alistawi zaidi katika miaka ya 1970 na 1980.
Anajulikana zaidi kama mmoja wa waimbaji wakuu wa bendi ya TP OK Jazz ya Kongo ambayo ilikuwa bendi maarufu zaidi barani Afrika katika miaka ya 1980.
Alizaliwa Oktoba 30, 1946 huko Kinsiona, Bas Congo. Vipaji vyake vya muziki vilianza kujitokeza pale alipojiunga na kwaya ya shule hiyo, na kuigiza peke yake nyimbo mbalimbali za kwaya hiyo. Baada ya kumaliza shule kuwa mwalimu, akifundisha katika mzunguko wa d’Orientation (CO). Baada ya kufundisha kwa mwaka mmoja, aliondoka na kuendelea na kazi ya muziki.
Mnamo mwaka wa 1966, alijipa Dalienst ya sobriquet, mchezo wa jina lake la Kikristo, na jina lake la mwisho. Mnamo 1967 alijiunga na Vox Africa ambayo ilikuwa mojawapo ya bendi za juu nchini, Zaire wakati huo, ikiongozwa na Jeannot Bombenga.
Na mwaka 1968 alijiunga na bendi ya Festival Des Maquisards iliyokuwa ikiongozwa na Sam Mangwana, ambaye hivi karibuni alikuwa ametoka katika bendi ya Tabu Ley Africa Fiesta National, Maquisards wakati huo ilikuwa moja ya bendi maarufu nchini Zaire na ilikuwa na vipaji vya aina yake Sam Mangwana, Mavatiku Michelino, Dizzy Madjeku. , Jerry Dialungana, Lokombe Ntal na Kiese Diambu ambaye alikuwa binamu wa Dalienst. Washiriki wote wa bendi walijizolea umaarufu mkubwa na TP OK Jazz.
Mnamo 1969, Maquisards waligawanyika na Mangwana kuondoka na kuunda kikundi chake, Dalienst na Dizzy walifikiria kujiunga tena na Vox Africa. Baadaye waliamua kumkaribia Verkys Kiamanguana kwa usaidizi wa Verkys, Maquisards ilifufuliwa kutoka kwenye kitanda chake cha kifo, Wanakuwa moja ya bendi kubwa nchini Kongo inayotoa albamu kadhaa kali kama vile Maria Mboka, Obotama Mobali na Tokosenga na Nzambe nyimbo zote zilizovuma. kutoka kwa Dalienst. Bendi hiyo ilikuwa sasa kama Grand Maquisards.
Miaka ya mapema ya 1970 ilikuwa miaka ya mafanikio makubwa kwa Maquisards huku kukiwa na vibao kama vile Mabala ya Kinshasa na Kaka po na ye ya Dizzy Mandjeku. Sonia ya Diana, Kayumba Martha, na Tolimbisana ya Lokombe, Jarrya na Kiesse Diambu, Mavata, Beneda na Sisi moke ya Dalienst
Kufikia 1974, bendi ilianza kuvunjika kwa sababu ya kutokukubaliana na Verkys. Walikaa mwaka mzima bila kutumbuiza au kuachia nyimbo zozote, na hatimaye bendi hiyo ikaporomoka mwaka wa 1975.
Alijiunga na TP OK Jazz mnamo Septemba 1978 kufuatia kuanguka kwa Macquisards pamoja na Jerry Dialungana. Ilichukua ushawishi mkubwa kutoka kwa Franco kumfanya Dalienst ajiunge, na alipoondoka OK Jazz miezi miwili baadaye, Franco bado alimshawishi kurudi.
Dalients alikuwa wimbo wa papo hapo katika TP OK Jazz, utunzi wake wa mwanzo mwishoni mwa miaka ya 1970 ulijumuisha nyimbo kama vile Tala Ye Na Miso (Mtazame kwa macho), Zaina Mopaya (Zaina the stranger) na Lisolo na Adamo na Nzambe (Mazungumzo ya Adam. na Mungu).
Katika wimbo huo, Dalienst alikumbuka jinsi tangu mwanzo wa wakati, wanaume huwalaumu wanawake kila wakati kwa shida zao wakati kwa kweli wanaume ndio wenye makosa. Wimbo huo haukupokelewa vyema na Makasisi wa Zaire ambao waliuona wimbo huo kuwa unashambulia dini yao. Wimbo huo ulikuwa wa kwanza kati ya nyingi zilizomletea Dalienst sifa ya kuwa mtetezi wa wanawake.
Wakati wanachama 10 wa TP OK Jazz walipokamatwa mwaka wa 1978 na kupelekwa katika gereza maarufu la Makala, Dalienst alikuwa mmoja wa washiriki wachache wa bendi hiyo waliotoroka kukamatwa. Alifaulu kumsadikisha mchungaji huyo kwamba hakuimba nyimbo zozote chafu zilizosababisha kukamatwa.
1980 ilishuhudia wimbo wa kwanza wa Dalienst ‘mega hits’ katika wimbo Liyanzi Ekoti Ngai Motema (Tick imeingia moyoni mwangu), wimbo huo ulijulikana kwa jina la Mouzi.

DAR ES SALAAM

Na Remigius Mmavele

Kundi la Makoma lilikuwa mshindi wa tuzo za pop, R&B na kikundi cha muziki wa dansi kilichotokea Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani Zaire) na kuanzishwa Uholanzi. Kundi hili linaundwa na ndugu 6 (kaka 3 na dada 3): Nathalie Makoma, Annie Makoma, Pengani Makoma, Tutala Makoma, Duma Makoma, Martin Makoma na asiye mwanafamilia, Patrick Badine. Waimbaji wa kundi la Makoma, wanaimba hasa kwa Kilingala na Kiingereza, lakini nyakati nyingine pia kwa Kifaransa, Kiholanzi na Kijerumani.
Kundi hili lilianzishwa mwaka 1993 kikiwa na waimbaji hao wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao walihamishia makazi yao nchini Uholanzi baada ya kukimbia migogoro ya kisiasa nchini kwao.
Awali kundi hili lilikuwa linaitwa “Nouveau Testament” kabla ya kubadilishwa jina na kuitwa Makoma baada ya kuanzishwa Ulaya. Kundi hili limetoa albamu kadhaa zikiwemo “Nzambe na Bomoyi” (1999), “On Faith” (2002), na “Na Nzambe Te, Na Bomoyi Te” (2005).
Kundi hili la muziki linaloimba nyimbo za dini za kumsifu na kumtukuza Mungu, limepokea sifa na tuzo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kundi Bora la Kiafrika katika Tuzo za Kora 2002. Baada ya kuwa pamoja kwa miaka mingi mwaka 2004 mmoja wa waimbaji viongozi katika kundi hilo Nathalie Makoma aliondoka kwenye kundi hilo na kuamua kuwa mwimbaji wa kujitegemea.
Baada ya kufahamu wasifu wa kundi hilo, sasa ni wakati wa kufahamu wasifu wa waimbaji mmoja mmoja wa kundi hilo la Makoma tukianza na mwimbaji Nathalie Makoma.
Nathalie Makoma alizaliwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1982. Nathalie Makoma ni mwimbaji mashuhuri wa Kongo Uholanzi, mtunzi wa nyimbo, na mtunzi wa televisheni ambaye alipata umaarufu baada ya kushiriki katika msimu wa nne wa toleo la Kiholanzi la “Idols.”
Kabla ya kazi yake ya muziki wa kujitegemea, Nathalie alikuwa mmoja wapo wa waimbaji wa kikundi cha injili kinachoitwa Utatu. Alitoa albamu yake ya kwanza, “Nathalie Makoma,” ambayo ilijumuisha wimbo wa “I Just Wanna Dance.” Nathalie ametoa albamu nyingine kadhaa na single na pia ameonekana kwenye programu mbalimbali za televisheni za Uholanzi. Kazi yake ya hisani ni pamoja na kusaidia mashirika kama vile UNICEF.
Mwimbaji mwingine ni Martin Makoma ambaye ni mwanamuziki mahiri wa Kongo, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mchungaji. Amechangia mafanikio ya kundi la Makoma na maonyesho yake makubwa na vipaji vya sauti. Zaidi ya hayo, anatambuliwa kama mchungaji wa jumuiya ya Kikristo mtandaoni inayoitwa Bethesda Ministry. Michango ya Martin inaendelea kuacha athari ya kudumu kwa tasnia ya muziki na ulimwengu wa imani.
Tutala Makoma naye ni mmojawapo ya waimbaji wa kundi hilo la Makoma, ni mwanamuziki na rapa wa nyimbo nyingi kutoka Kongo. Mnamo 1993, alianzisha kikundi cha muziki cha Makoma, ambacho kilipata umaarufu mkubwa.
Makoma inaadhimishwa kwa mitindo yake tofauti ya muziki inayojumuisha Kristu, pop, na R&B. Albamu yao ya kwanza, “Nzambe na Bomoyi” (Yesu kwa Uhai), ilitolewa mwaka wa 1999, kuashiria kuanzishwa kwa taswira yao yenye mafanikio. Usanii wa kufoka wa Tutala Makoma ulichangia kwa kiasi kikubwa utofauti wa utambulisho wa wanamuziki wa kundi hilo.
Zaidi ya shughuli zake za kimuziki, Tutala Makoma anavaa kofia za mtayarishaji mahiri na Afisa Mtendaji Mkuu wa Westcoassrecords. Ustadi wake wa utayarishaji umekuwa muhimu katika kutengeneza vibao vya Makoma Band na wanamuziki mbalimbali wanaotambulika. Umahiri wa ubunifu wa Tutala na uwezo wake wa kimuziki unaendelea kuwavutia mashabiki kote ulimwenguni, na kuacha athari ya kudumu kwa ulimwengu wa muziki.
Yupo pia, Duma Makoma ambaye ni rapa kutoka Kongo, mpiga midundo, akiwa na haiba ya kuambukiza na talanta ya kipekee ya muziki, Duma amejipatia umaarufu katika tasnia ya muziki. Amechangia ustadi wake wa kurap na uchezaji midundo kuunda mchanganyiko wa kipekee wa injili, R&B, na midundo ya Kiafrika. Muziki wa kuinua na kuhamasisha bendi hiyo umeifanya kutambulika kimataifa, kwa vibao kama vile “Napesi” na “Mokonzi Na Bakonzi.” Beti za kufoka zenye nguvu za Duma na uchezaji wa mdundo wa mdundo umekuwa sahihi ya sauti ya Makoma. Kupitia muziki wao, Duma Makoma wanaendelea kuhamasisha na kuvutia hadhira duniani kote.
Mwingine ni Annie Makoma, katika bendi hii ya familia ni Annie mke wa mwimbaji Patrick Badine. Juhudi zao za pamoja zimezaa nyimbo na albamu nyingi, kama vile “Napesi,” “Moto Oyo,” na “Mwinda.” Uwezo wa kipekee wa sauti wa Annie Makoma na uwepo wa jukwaa la kuvutia umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio makubwa ya kikundi.
Safari yake ya muziki imemfikisha katika hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuonekana kwenye fainali ya Uholanzi Idols pamoja na ndugu zake. Kote ulimwenguni, Annie Makoma anaendelea kuvutia na kuhamasisha hadhira kupitia usanii wake na maonyesho ya kuvutia.
Patrick Badine ni mwanamuziki mahiri na mwanachama wa kundi maarufu la muziki la Makoma ambaye anatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa uwepo wake wa ajabu wa jukwaa, Patrick amevutia watazamaji ulimwenguni kote.
Huyu sio mwanafamilia kwa maana sio ndugu katika familia ya Makoma kama ilivyokuwa kwa waimbaji wengine bali ni mume wa Annie Makoma hivyo ni shemeji yao wanafamilia wengine wanaounda kundi hilo la Makoma.

Budapest, Hungury
Riadha ya Dunia imetoa ulinzi wa mwaka mzima kwa wanariadha 25 kwenye baadhi ya majukwaa yao ya mitandao ya kijamii, kwa kutumia akili ya bandia, baada ya kutambuliwa kama watu wanaolengwa sana kwa unyanyasaji wakati wa hafla kuu.
Baraza linaloongoza, limeendesha utafiti katika kipindi cha miaka minne iliyopita, unaojumuisha Michezo miwili ya Olimpiki na Mashindano mawili ya Dunia, ili kuchanganua matumizi mabaya ya mtandaoni kwa wanariadha wake.
Zaidi ya machapisho au maoni milioni 1.4 yalichanganuliwa, yakijumuisha wachezaji 2,438 wa riadha, uwanjani na barabarani.
Utafiti huo ulijumuisha maoni na unyanyasaji uliolengwa ambapo wanariadha walitambulishwa, lakini haujumuishi ujumbe wa moja kwa moja au unyanyasaji usiolengwa.
Riadha ya Dunia haijawatambua wanariadha 25, na kusema kwamba msaada huo utapanuliwa mwaka ujao.
“Tumewekeza rasilimali kubwa katika kufanya utafiti kuhusu unyanyasaji mtandaoni na mojawapo ya mafanikio yetu makubwa kutokana na mpango huu, ni uwezo wetu wa kutoa msaada kwa wanariadha na kuwapa zana za kujilinda dhidi ya unyanyasaji mtandaoni”, alisema rais wa Riadha wa Dunia Lord Coe.

BARCELONA, Hispania
Christopher Nkunku ndilo jina jipya linaloonekana katika chaguzi za klabu ya soka ya Barcelona, ili kuimarisha msimamo wa mrengo wa mradi ujao wa michezo.
Mchezaji huyo wa Ufaransa anataka kuondoka Chelsea kutokana na kutokuwa na umaarufu, na anatafuta timu ya kiwango cha juu ambayo itampa dakika za kurejesha toleo la kuvutia alilotoa Leipzig, na kumfanya kuwa mmoja wa wanasoka wanaotafutwa sana sokoni.
Jina lake limetolewa na wakala wake, Pini Zahavi, ambaye ana uhusiano mzuri na klabu ya Blaugrana, na atakuwa tayari kurekebisha mshahara wake ikibidi.
Angependa kuondoka sasa, lakini Barca haina mpango wa kwenda soko la Januari kutokana na matatizo yake ya mishahara.
Nkunku alikuwa mmoja wa wachezaji wakubwa waliosajiliwa na Chelsea katika msimu wa joto wa 2023, na waliwekeza Euro milioni 60 kwa mmoja wa wachezaji tofauti katika Ligi ya Mabingwa, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa hajaondoka katika klabu hiyo ya London.
Chelsea, ikiwa na idadi kubwa ya wachezaji katika safu zake zote, itakuwa tayari kumfungulia milango.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Klabu ya soka ya Singida Black Stars imesema mradi wake wa kujenga uwanja wao mpya, umefikia asilimia 95 kukamilika ili waanze ujenzi.
Afisa Habari wa Klabu hiyo Hussein Massanza (pichani) amesema kwamba wapo katika hatua nzuri ya ujenzi huo ili kumiliki uwanja watakaoutumia katika michezo yao ya nyumbani.
Alisema kwamba uwanja huo utajengwa Singida, ambapo ukikamilika wataachana na matumizi ya uwanja wa CCM Liti, ingawa hawatouacha rasmi kwa sababu watautumia mara chache pale itakapowalazimu kufanya hivyo.
“Tumemsikia Rais wa TFF Wallace Karia akisisitiza Klabu za Ligi Kuu kuwa na viwanja vyao vya mazoezi.Sisi huko tayari tulishakufikiria, na tunaendelea na mchakato,”alisema.
Kwa upande wa kiwanja cha mazoezi, Massanza aliongeza kuwa wana mpango wa kujenga viwanja vya mazoezi mkoani Singida ili kutimiza takwa la Leseni za Vilabu ambalo mara zote Shirikisho la Soka Duniani (Federation of International Football Associations: FIFA) limekuwa ikisisitiza.
“Sisi ni timu kubwa, tunataka kuwa na uwanja wetu, tuwe na viwanja vingine vya mazoezi ambavyo timu zetu zitakuwa zinatumia, ikiwemo za vijana,”alisema.
Alisema kwamba wanataka timu yao iwe bora katika maeneo yote, na si uwanjani pekee.