Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Mwanza

Na Paul Mabuga

Maandishi yaliyoandikwa kwenye bajaji zetu, ambayo  kwa  muhtasari na kwa  muktadha wa yaliyokusanywa katika makala haya, unaweza kusema ni kama kutoka, “Enzi za Mwalimu” hadi “Kwenye Ndoa Yenu...”:, na vilevile ni maneno yanayosema mengi yenye kusisimua, kuibua hisia, kufurahisha na hata kufikirisha, sembuse kutia hofu na kuogofya.

Ni kwamba licha ya barabara za miji yetu hapa nchini, kujaa watu na shamrashamra za kelele za honi, lakini  pia zimesheheni  falsafa ya Mswahili.. Sio kwenye vitabu au kwenye mikutano ya hadhara, bali kwenye mabango madogo yaliyobandikwa, au kuandikwa nyuma ya magari yetu ya usafiri, na vyombo vingine maarufu kama Bajaji.

Dekano wa Dekania ya Kilimahewa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Paul Kamuhabwa akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliopata Sakramenti Takatifu ya Kipaimara wa Parokia ya Bikira Maria Malkia-Kilimahewa jimboni humo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo. Mstari wa nyuma ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Daudi Ngate.

Dar es Salaam

Na Pd. Richard Mjigwa- C.PP.S

Ilikuwa ni Novemba 8, mwaka 1984, Mtakatifu Yohane Paulo II (Papa), alipochapisha Waraka unaojulikana kama “Tot tantaeque” yaani “Bikira Maria ameidhinishwa kuwa Mlinzi na Mwombezi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, Sherehe inayoadhimishwa kitaifa kila mwaka ifikapo Desemba 9.
Katika mkesha wa uhuru wa Tanganyika, Mtakatifu Yohane XXIII, alitunga Sala Maalumu kwa ajili ya kuiombea Tanganyika, ili uhuru wake uweze kuwanufaisha watu wake.

DAR ES SALAAM

Na Edvesta Tarimo

Afya ya akili ni moja ya vipengele muhimu zaidi vya ustawi wa binadamu, lakini mara nyingi hupewa nafasi ndogo katika mjadala wa afya. 
Hata hivyo utafiti unaonesha kwamba, afya ya akili inajumuisha hali ya kiakili, kihisia na kijamii ya mtu, na ni msingi wa jinsi anavyokabiliana na changamoto za kila siku. 
Licha ya kwamba kila mtu anapitia magumu maishani, kuna njia za kujikinga dhidi ya athari za majeraha ya kihisia (kiwewe), na kujenga uthabiti wa kukabiliana na hali ngumu.

Waimarishwa wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara wa Parokia ya Mtakatifu Maria Magdalena – Kimara Mtoni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Joseph Cottolengo – Masaki - Kisarawe, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (mwenye Fimbo ya Kichungaji) akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Parokia ya Mtakatifu Teresa wa Calcutta - Kivule, baada Adhimisho la Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa na Altare.

Masista wa Shirika la Dada Wadogo wa Mtakatifu Fransisko wa Asizi Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Nadhiri za Daima na Jubilei ya Miaka 25 ya Utawa iliyofanyika hivi karibuni.

Mwanza

Na Paul Charles Mabuga 

Kichapo cha 2-0 kutoka kwa Azam FC, si tu kwamba kimepunguza kasi ya Simba kwenye mbio za ubingwa, bali kimetupa picha ya kutisha: Simba inaumwa, na wapinzani wamegundua dawa ya ugonjwa wake.

Matokeo haya yanazua swali gumu: Je, timu hii imegeuka kuwa Mnyama wa Karatasi? Uchambuzi huu unakwenda ndani kabisa, ukifichua kwa nini udhaifu mmoja unajirudia, na jinsi benchi la ufundi linavyoshindwa kuleta ufumbuzi, dhidi ya mbinu za kisasa za mpinzani. Hii ni muhimu kwa kuwa timu imefungwa namna ile ile, kama ilivyotokea kwa Stade Malien.

DAR ES SALAAM

Na Remigius Mmavele

Papy Tex mwimbaji mwenye sauti ya kuvutia na ya kipekee jina lake lake halisi ni Matolu Dode Jean , alizaliwa Juni 28, 1952 katika jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Baba yake mzazi alikuwa ni raia wa nchi ya Angola na mama yake kutoka Kongo ya Kati, alilelewa na Joséphine Matolu. Ni mwanamuziki maarufu duniani, mwandishi , mtunzi na mtayarishi wa muziki ambaye sauti yake ya huzuni na nyimbo zake zimeacha alama katika fikra za watu na bado zinaacha kumbukumbu zisizofutika katika kumbukumbu ya pamoja.