Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

DODOMA

Na Mwandishi Maalum

Serikali imegawa mashine mpya 185 zenye thamani ya Shilingi bilioni saba  kwa ajili ya uchunguzi na ugunduzi wa vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu ili kutokomeza ugonjwa huo nchini, ifikapo mwaka 2030.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, kwenye hafla ya ugawaji wa mashine hizo iliyofanyika katika Kituo cha Afya Chamwino, Dodoma, iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mpango Harakishi wa Kuibua Wagonjwa wa Kifua Kikuu katika Halmashauri 76 za Mikoa tisa.
Waziri Mhagama alisema kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, ambapo kwa sasa ni nchi ya sita kati ya nchi zote zinazofanya vizuri, lakini bado juhudi zinaendelea ili kufanya vizuri zaidi kwa kuwa bado tupo ndani ya nchi 30 zenye maambukizi makubwa.
“Ugonjwa wa Kifua Kikuu bado ni ugonjwa tishio nchini na ulimwenguni kwa ujumla, kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa huo, ambazo kwa pamoja zinachangia asilimia 87 ya wagonjwa wote wa Kifua Kikuu Duniani,” alisema Waziri Mhagama.
Alisema, “Tanzania ilikadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Kifua Kikuu 122,000, ikiwa ni sawa na wagonjwa 183 kwa kila watu 100,000, ambapo kwa mwaka 2023, Tanzania iliweza kugundua na kuwaweka katika matibabu wagonjwa 93,250, ikiwa ni sawa na asilimia 76 ya wagonjwa 122,000 waliokadiriwa na Shirika la Afya Duniani (World Health Organization: WHO) kuwepo nchini.
Alisema kuwa hali hiyo imeleta msukumo mkubwa ndani ya Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta katika kuongeza juhudi za kupambana na Kifua Kikuu.
Kwa kuzindua mashine hizo, Tanzania inaendelea kuimarisha mtandao wa huduma za uchunguzi na ugunduzi wa vimelea vya Kifua Kikuu kwa njia ya vinasaba ambapo sasa kutakuwa na jumla ya mashine 569 zenye uwezo wa kupima vimelea vya Kifua Kikuu pamoja na usugu wa dawa kutoka mashine 384 zilizokuwepo mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 48.
Katika hatua nyingine Waziri Jenista alizindua Mpango Harakishi wa Kuibua Wagonjwa wa Kifua Kikuu kwenye Halmashauri 76 katika Mikoa 9, amabyo kwa 2024 imeonyesha kuwa na kiwango kidogo cha uibuaji wa wagonjwa, ikilinganishwa na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Waziri Jenista aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Kagera, Mara, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu na Tanga
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janeth Mayanja, aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.
Alisema kuwa mashine hizo zilizotolewa, zitakwenda kusaidia katika utambuzi wa mapema wa wagonjwa wa Kifua Kikuu, hivyo kuibua watu wengi zaidi wanaougua ugonjwa huo, na kupata tiba mapema.
Naye Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Ahmad Makuwani alisema kwamba licha ya ugonjwa huo kuendelea kuwa tishio, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na Kifua Kikuu, ikiwa ni miongoni mwa nchi sita (6) zinazofanya vyema katika mapambano.
Dk. Makuwani alisema kuwa juhudi kubwa sasa zinaelekezwa katika uibuaji wa wagonjwa wapya wa Kifua Kikuu, na Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika teknolojia ya matibabu, hasa kwenye vifaatiba, hivyo sasa tuna jukumu la kutoacha mtu nyuma kwenye mapambano hayo ya kutokomeza Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030.

AUSHA

Na Mwandishi Maalum-PMO

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amesema kuwa Sekta ya Maliasili na Utalii ni chanzo kikubwa cha mapato ya Taifa kwa kuwa inahusisha shughuli nyingi za kiuchumi.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali itaendelea kubuni mikakati ya kuimarisha sekta ya Maliasili na Utalii kwa kuwa sekta hiyo ni nguzo muhimu kwa uchumi wa Taifa.
Alisema hayo wakati alipozindua Tuzo za Uhifadhi na Utalii katika Ukumbi wa Hoteli ya Mt. Meru, jijini Arusha.
“Sekta hii peke yake inachangia asilimia 21.5 katika pato ghafi la Taifa ambapo asilimia 17.2 ni utalii, asilimia 4.3 ni misitu na nyuki,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha, alisema kuwa Sekta hiyo inachangia asilimia 30.9 ya mapato ya fedha za kigeni, ambapo asilimia 25 yanatokana na utalii na asilimia 5.9 ni kutoka misitu na nyuki.
Katika hatua nyingine, Majaliwa alisema kuwa juhudi za dhati na maono makubwa ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuiendeleza Sekta ya Maliasili na Utalii, yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa kwa asilimia 96 kutoka watalii 922,692 mwaka 2021 hadi watalii 1,808,205, mwaka 2023.
Waziri Mkuu Majaliwa aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaweka vigezo vya wazi na vinavyojulikana vya uteuzi na upokeaji wa tuzo.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana alimpongeza Rais Dk. Samia kwa namna anavyojitoa katika kuhakikisha Sekta ya Maliasili na Utalii inaendelea kukua kwa kasi.
Aliongeza kuwa Wizara hiyo imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuimarisha uhifadhi na kuendeleza utalii, ikiwemo kutumia teknolojia mbalimbali pamoja na kuendeleza Programu ya Tanzania – “The Royal Tour” na kuibua mazao mapya ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii.

DODOMA

Na Mwandishi wetu

Serikali ya Tanzania imeihakikishia Serikali ya Uingereza kuendeleza ushirikiano kwenye Sekta ya madini, hususan katika kujengea uwezo Watu wake.
Mpango huo unakwenda sanjari na kubadilishana uzoefu, uongezaji thamani madini, na kuwekeza kwenye kufanya utafiti mbalimbali ili kukuza Sekta hiyo na kupanua mnyororo wa thamani,i kuongeza ajira na kuchangia ukuaji Pato la Taifa.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (pichani), Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mh. Marianne Young.
Katika mazungumzo hayo, Tanzania na Uingereza zimekubaliana katika kuwajengea uwezo Watu wake na kubadilishana uzoefu, hususan katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini nchini, Gst.
Aidha, itashirikiana na British Geological Survey, Bgs, ya Uingereza, ili kuwajengea uwezo Watanzania kwa kuwa na ujuzi stahiki katika masuala ya uendelezaji wa Sekta ya Madini.
Mavunde alisema, Uingereza pia imeonesha utayari katika kushirikiana na Tanzania katika eneo la mnyororo mzima wa uongezaji thamani madini, mkakati ambapo Tanzania imejipanga kuhakikisha inavutia uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini hapa nchini.
Naye Balozi Marriane Young, alipongeza jitihada kubwa za kukuza Sekta ya Madini zinazofanywa na Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na kuahidi kuimarisha ushirikiano mkubwa baina ya nchi hizo, hasa katika kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo kupitia Taasisi za madini za nchini Uingereza na Tanzania.
Balozi Young ameunga mkono mpango wa uongezaji thamani madini nchini, na kuahidi kwamba Uingereza itashirikiana na Tanzania kwa ukaribu ili malengo hayo yatimie.

DAR ES SALAAM

Na Angela Kibwana

Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (United Nations International Childrens Emergence Fund: UNICEF) limezindua Ripoti yake mpya ya Majibu ya Kibinadamu yenye ombi la kuchangisha fedha dola bilioni 9.9 ili kufikia watoto milioni 109 katika nchi 146 kwa msaada wa kuokoa maisha kwa mwaka wa 2025.
Fedha hizo zitatumika kukabiliana na shida za kibinadamu, kutokana na  migogoro mingi, majanga ya tabianchi na kuyahama makazi yao na majanga ya kiafya yanatarajiwa mwaka ujao.
Ulimwenguni kote, watoto milioni 213 wanakabiliwa na dharura za kibinadamu zisizotabirika na zinazobadilika kila wakati. Huku ikiwa na watoto milioni 109 ambao UNICEF inawapangia msaada wa kibinadamu kwa mwaka 2025, ufadhili wa kifadhili ni muhimu ili kuhakikisha mwitikio huo unapatikana kwa wakati, thabiti na wa kutosha.
Hayo yamethibitishwa katika Ripoti mpya iliyozinduliwa na UNICEF Desemba 5 mwaka 2024.
“Kiwango cha mahitaji ya kibinadamu ya watoto kiko katika kiwango cha juu kihistoria, huku watoto wengi wakiathirika kila siku,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF,  Catherine Russell na kuongeza,
“Tukiangalia mbele hadi 2025, tunakadiria kuwa watoto milioni 213 katika nchi na wilaya 146 watahitaji usaidizi wa kibinadamu katika kipindi cha mwaka - idadi kubwa. Ni kazi ya UNICEF kufikia kila mmoja wa watoto hawa na huduma muhimu na vifaa wanavyohitaji, na kuhakikisha kwamba haki zao zinalindwa na kuzingatiwa – jukumu ambalo limeongoza kazi yetu kwa miaka 78 iliyopita.”
Watoto milioni 57.5 wazaliwa nchi za migogoro:
Zaidi ya hayo, mnamo 2024, zaidi ya watoto milioni 57.5 walizaliwa katika nchi zilizoathiriwa na migogoro au machafuko mengine ya kibinadamu, ambapo UNICEF ilitoa rufaa ya dharura.
Idadi hii inatarajiwa kuongezeka kwa angalau vitengo 400,000 katika 2025. Wito kwa ajili ya  dola bilioni 9.9 kwa mwaka 2025, inaakisi  hitaji la dharura la kukabiliana na changamoto zinazoongezeka za kibinadamu zinazowakabili watoto katika nchi 146.
Katika mwaka 2023 wafadhili walichangia zaidi ya 50% ya ufadhili wa kimaudhui wa UNICEF katika dharura nne tu - Afghanistan, Ethiopia, Syria na Ukraine - sehemu ya dharura 412 ambazo UNICEF ilijibu katika nchi 107.
“Kusaidia rasilimali za kibinadamu za UNICEF zinazobadilika na kutoka ngazi ya chini, ni muhimu kwa kazi yetu na watoto walioathiriwa na majanga,” alisema Russell na kuongeza,
“Fikiria kile tunachoweza kufikia kwa watoto kwa kufanya kazi pamoja kupitia hatua za maana za kibinadamu, kuunda ulimwengu ambapo haki za kila mtoto zinalindwa na kuungwa mkono, na ambapo kila mtoto anaweza kukua na kustawi - ulimwengu ambao unafaa kila mtoto”.
Aidha, ripoti hiyo ilibainisha kuwa wakati huo huo, oparesheni za kibinadamu katika nchi kama vile Burkina Faso, Lebanon, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,(DRC) Mali na Myanmar, zimekuwa zikikosa fedha nyingi zaidi.

LUSAKA, Zambia

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amelishukuru Kanisa Katoliki nchini humo kwa kuunga mkono juhudi za kurekebisha na kupunguza madeni nchini humo.
Katika ziara ya Balozi wa Vatican katika Makao Makuu ya Rais huyo hivi karibuni, Rais Hichilema alitambua jukumu lililofanywa na Kanisa Katoliki katika kuunga mkono juhudi za kurekebisha deni la Zambia, akibainisha kwamba michango ya Kanisa inaendana na malengo ya Zambia kupunguza madeni na kufufua uchumi.
Hiyo ilifuata katika kushukuru Ujumbe wa 58 wa Amani Duniani wa Baba Mtakatifu Fransisko unaoongozwa na kauli mbiu: “Utusamehe makosa yetu, Utupe Amani.”
Katika fursa hiyo, Rais wa Zambia Bwana Hakainde Hichilema alitaka kutoa heshima wakati wa mkutano wake na Balozi wa Vatican huko Lusaka nchini humo, Askofu Mkuu Gianluca Perici.
Katika mkutano huo, Rais Hichilema alitambua hasa jukumu muhimu lililofanywa na Kanisa Katoliki katika kuunga mkono juhudi za kurekebisha deni la Zambia, huku akibainisha kwamba michango ya Kanisa inaendana na malengo ya Zambia ya kupunguza madeni na kufufua uchumi.
Hiyo ni pamoja na kuunga mkono nafasi ya Zambia katika mfumo wa msamaha wa madeni wa G20, ambapo Rais Hichilema alisisitiza kuwa utawala wake umejitolea kuwekeza kiasi kinachotokana na msamaha wa madeni katika uwekezaji wa kimkakati na ushirikiano wa kibiashara wa kimataifa, ili kukuza maendeleo ya nchi.
Katika hotuba yake, Hichilema alisisitiza dhamira ya Serikali ya kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya kidini, hasa Kanisa Katoliki, ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu, afya na ustawi wa jamii nchini Zambia.
Rais huyo alisisitiza kuwa sera shirikishi ya Zambia ya kushirikiana na Mashirika ya Kidini, ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha ustawi wa raia wa nchi hiyo.
Balozi wa Vatican nchini Zambia, Askofu Mkuu Perici aliwasilisha kwa Rais ujumbe maalum kutoka kwa Baba Mtakatifu Fransisko, huku akielezea shukrani kwa juhudi za Zambia katika mchakato wa kurekebisha madeni.
Ujumbe huo, kwa kuzingatia Siku ya 58 ya Amani Duniani, kwa hakika unahimiza ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali ya Zambia, na kwamba Baba Mtakatifu Fransisko aliakisi mada za amani, maelewano na msamaha wa madeni, huku akitoa wito wa kuimarisha uhusiano kati ya Vatican na Zambia, na zaidi hata hisia alizoshiriki wakati wa ziara ya Rais Hichilema mjini Vatican mnamo mwaka 2022.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa nchini Zambia, Mulambo Haimbe aliongeza kusema kuwa ujumbe wa Papa Fransisko ni kielelezo cha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia wa Zambia na Vatican, ambayo itaadhimisha miaka 60 mwaka huu 2025 tangu ulipoanzishwa uhusiano huo.

LUSAKA, Zambia
Wakristo wamekumbushwa kuwa waaminifu wakimwamini Mungu, hata wakati wa changamoto za maisha wanazokutana nazo kila wakati.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Lusaka nchini Zambia, Mhashamu Sana Alick Banda (pichani) alipokuwa akitoa ujumbe kwa Waamini jimboni humo.
Wakati huo huo, aligusia pia kuhusu Sikukuu ya Noeli, akisema, “Krismasi inazungumza kwa sauti kubwa na wazi. Mungu hajaacha wala kutuacha.
Kuzaliwa kwa Yesu kunaonyesha kwamba utukufu wa Mungu haupatikani katika utajiri, pomp, au kelele za ulimwengu, lakini kati ya watu wake - masikini, wa chini, na mateso.”
Aliongeza kwamba kuzaliwa kwa Yesu ni ushuhuda kwa uaminifu wa Mungu usio na wasiwasi, akisema, “Katika mtoto aliyevikwa nguo za kuvinjari na kuwekewa manyoya, kuna utimilifu wa kila ahadi ya tumaini.” Kutafakari juu ya mfano wa Mtakatifu Joseph, Askofu Mkuu Banda aliwasihi mkutano wa kumwamini Mungu, haswa katika wakati mgumu.
Aidha, alibainisha kuwa mfano wa Joseph unawaalika kumtegemea Mungu wakati maisha yanapokuwa mazito wakati wanapokabiliwa na gharama za kuishi, ukosefu wa ajira, na mapambano ya kutoa familia zao.

KAMPALA, Uganda
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Uganda (Uganda Episcopal Conference: UEC), Askofu Anthony Joseph Zziwa (pichani kulia), ametoa wito wa kuzingatiwa upya kwa familia kama msingi wa jamii.
Aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu, huku Maaskofu nchini humo wakizitaka familia kutafakari wajibu wao katika kukuza upendo, amani na utulivu, sambamba na kielelezo kilichotolewa na Familia Takatifu ya Nazareti.

VATICAN CITY, Vatican

Baba Mtakatifu Fransisko amekutana na Wanachama wa Chama cha Umoja wa Wasioona na wenye Ulemavu wa Macho (Vipofu) nchini Italia.
Pande hizo mbili zimekutana katika ukumbi wa Clementina, mjini Vatican, akiwaalika kutembea na kuwa Mahujaji wa Matumaini kama vile Pier Giorgio Frassati, Francis na Clara wa Assisi, au Teresa wa Mtoto Yesu.
Aliwahimiza kutambua kwamba kinachowategemeza katika juhudi zao ni lengo la mwisho, yaani ahadi ya kuwepo kwa upya ndani ya Yesu, ambaye hutoa furaha tofauti ambayo haibaki nje au juu ya uso.
Papa aliwatakia Wanachama hao heri ya Mwaka Mpya, akisema, “Uwe mwaka wa ukuaji wa kibinafsi, na pia katika urafiki kati yenu.”
Vile vile, aliwasihi kufikiri na kujichukulia kama ni watu wanaotembea, na walioko kwenye safari, na kwamba katika kila umri, watoto, vijana, watu wazima, wazee, daima wawe ni watu wa kusonga mbele bila kukata tamaa.

VATICAN CITY, Vatican

Baba Mtakatifu Fransisko amekemea vitendo vya kuwanyanyasa watoto, ikiwemo kuwanyima haki ya kupata elimu.
Baba Mtakatifu alisema hayo hivi karibuni alipokutana na Chama cha Waalimu wa Kikatoliki cha Italia (Italian Association of Catholic Teachers: AIMC), Umoja wa Waalimu wa Kikatoliki wa Italia, Wasimamizi, Waelimishaji, Wakufunzi (UCIID), pamoja na Chama cha Wazazi wa Shule za Kikatoliki (AGESC).
Alisema kwamba ni furaha yake kuona Maadhimisho ya Mashirika yao, Miaka 80 ya Chama cha Waalimu Wakatoliki wa Italia na Umoja wa Waalimu wa Kikatoliki wa Italia, Wasimamizi, Waelimishaji, Wakufunzi, na Miaka 50 ya Umoja wa Wazazi wa Shule za Kikatoliki.
Aidha, Baba Mtakatifu alibainisha kwamba anaumia kuona watoto ambao hawajasoma na kwenda kazini, mara nyingi wanatumikishwa au kwenda kutafuta chakula au vitu vya kuuza katika mazingira yasiyoridhisha.
“Ninaumia kuona watoto ambao hawajasoma na kwenda kazini,mara nyingi wanatumikishwa au kwenda kutafuta chakula, au vitu vya kuuza mahali palipo na takataka,” alisema Baba Mtakatifu.
Sambamba na hayo, Papa aliongeza, “Ni fursa nzuri ya kusherehekea pamoja na kukumbuka historia yao na kutazama siku zijazo. Zoezi hili, harakati hii kati ya mizizi - kumbukumbu - na matunda - matokeo - ni msingi wa kujitolea katika uwanja wa elimu.”
Aliwaeleza kuwa kama mwalimu anayeingia katika ulimwengu wa wanafunzi wake, Mungu anachagua kuishi kati ya wanadamu ili kufundisha kupitia lugha ya uzima na upendo.
Aliongeza kwamba hiyo inawaita kwenye ufundishaji unaothamini mambo muhimu, na kuweka unyenyekevu, ukarimu na huruma katikati, na kwamba ualimu ulio na mbali na watu, haufai, na hausaidii.
Baba Mtakatifu alibainisha kwamba ualimu huo ni mwaliko wa kutambua utu wa kila mtu, kuanzia wale waliotupwa na walio pembezoni, jinsi wachungaji walivyotendewa miaka elfu mbili iliyopita, na kufahamu thamani ya kila awamu ya maisha, ikiwa ni pamoja na utoto.
“Matumaini yake si ya kipuuzi, yamejikita katika uhalisia, yakiungwa mkono na imani kwamba kila juhudi ya elimu ina thamani, na kwamba kila mtu ana utu na wito unaostahili kukuzwa,”alisema Baba Mtakatifu Fransisko na kuongeza,
 “Matumaini ndiyo injini inayomuunga mkono mwalimu katika kujitolea kwake kila siku, hata katika shida na kushindwa. Lakini tunawezaje kupoteza tumaini na kumwilisha kila siku? Kuweka mtazamo kwa Yesu, mwalimu na msindikizaji wetu njiani. Hii inatuwezesha kuwa kweli Mahujaji wa Matumaini.”
Aliwasisitiza kwamba wasisahau kamwe walikotoka, lakini wasitembee kwa kuinamisha vichwa chini kwa majuto, wakijutia nyakati nzuri zilizopita, badala yake wafikirie juu ya sasa ya shule ambayo ni mustakabali wa jamii, ikikabiliana na mabadiliko ya nyakati.

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Maadhimisho ya Jubilei Kuu ya Miaka 2025 ya Ukristo, yananogeshwa na kauli mbiu “Mahujaji wa Matumaini.
Matumaini ya Waamini yako katika Msalaba, yaani katika Kristo Yesu, chemchemi ya wokovu wa mwanadamu aliyezaliwa katika Familia Takatifu iliyopata baraka ya kuwa na Mungu, yaani Emanueli, kati yake.
Maadhimisho ya Sikukuu ya Familia Takatifu Desemba 29, mwaka 2024, imekuwa ni fursa kwa Majimbo kufungua lango la Maadhimisho ya Jubilei Kuu.
Baba Mtakatifu Francisko, katika mkesha wa Noeli tarehe 24 Desemba 2024, amefungua Lango Kuu la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, mwanzo wa maadhimisho ya Jubilei Kuu ya Miaka 2025 ya Ukristo. Hili ni Lango la matumaini, chemchemi ya watu wote wa Mungu.
Maadhimisho ya Jubilei ni kwa ajili ya watu wote, ili kuwaonjesha tena matumaini ya Injili, matumaini ya mapendo na matumaini ya msamaha wa kweli. Pango la Noeli ni ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu kwa binadamu; chemchemi ya matumaini; upendo wa Mungu unaovunjilia mbali ukaidi wa mwanadamu pamoja na hofu yake, tayari kutafakari ukuu wa matumaini yaliyo mbele ya mwanadamu. Mwelekeo huu, uwe ni mwangaza wa mapito ya kila siku ya mwanadamu.
Ni katika muktadha wa usiku huu ambapo “Lango Takatifu” la Moyo wa Mungu limefunguliwa. Kristo Yesu, Mungu pamoja nasi, anazaliwa kwa ajili ya binadamu wote.
Kumbe, pamoja naye, furaha ya dunia inachanua kama “maua ya kondeni.” Pamoja na Kristo Yesu, maisha yanabadilika na pamoja na Kristo Yesu “Spes non confundit” yaani “Tumaini halitahayarishi.” Rum, 5:5.
Maadhimisho ya Jubilei Kuu ya Miaka 2025 ya Ukristo yananogeshwa na kauli mbiu “Mahujaji katika Matumaini.” Matumaini ya Waamini yako katika Msalaba, yaani katika Kristo Yesu, chemchemi ya wokovu wa mwanadamu aliyezaliwa katika Familia Takatifu iliyopata baraka ya kuwa na Mungu, yaani Emanueli kati yake. Maadhimisho ya Sikukuu ya Familia Takatifu Desemba 29, 2024 imekuwa ni fursa kwa Majimbo mbalimbali duniani kufungua lango la Maadhimisho ya Jubilei Kuu ya Miaka 2025 ya Ukristo.
Januari Mosi mwaka 2025 itakuwa ni fursa kwa Parokia kufungua maadhimisho haya. Huu ni wito wa kutangaza na kushuhudia Imani yao kwa Kristo Yesu, Mlango wa uzima wa milele, na hivyo Wakristo wote wanaalikwa kuwa ni Mahujaji wa Matumaini yasiyo danganya; umoja unaopaswa kuimarishwa; kukuza na kujenga haki, amani na furaha ya kweli katika Kristo Yesu.
Kristo Yesu ndiye Lango la maisha ya uzima wa milele, anayewashirikisha waja wake Fumbo la upendo na huruma ya Mungu isiyokuwa na mipaka; huruma inayowakumbatia binadamu wote pasi na ubaguzi, changamoto na mwaliko wa kuambata toba, wongofu wa ndani na utakatifu wa maisha.
Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, katika Ibada ya kufungua Maadhimisho ya Mwaka wa Jubilei Kuu ya Mwaka 2025 ya Ukristo, amewataka watu wa Mungu kuzingatia mambo makuu manne, Kuzama zaidi katika kusoma, kutafakari na kuyaishi Maandiko Matakatifu.
Waamini wajitanabaishe kwa maisha yao ya Kikatoliki na hivyo kuachana na tabia ya kuwayawaya, kwani kwenye Kanisa Moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume, kuna kila kitu Waamini wanachohitaji katika maisha yao ya kiroho, sanjari na wokovu. Zaidi soma Tumaini Letu