Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

LUSAKA, Zambia

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zambia (Zambia Conference of Catholic Bishops: ZCCB) limezindua Kampeni ya kufuta madeni ya Mwaka wa Jubilei 2025, ikitoa wito wa msamaha wa haraka wa deni, haki ya kiuchumi, na uwazi katika usimamizi wa madeni ya Zambia.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Kapingila House mjini Lusaka nchini humo mwishoni mwa Mkutano wa Kwanza wa Baraza Kuu wa ZCCB kwa 2025, iliyokwenda na wito wa Baba Mtakatifu Fransisko wa haki ya kiuchumi na msamaha wa madeni duniani kote kama sehemu ya Mwaka wa Jubilei 2025.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais wa ZCCB, Askofu Mkuu Ignatius Chama wa Jimbo Kuu Katoliki la Kasama, alisisitiza tena msingi wa Kibiblia wa mapokeo ya Jubilei, akinukuu kitabu cha Mambo ya Walawi, 25:1-8 kinachosisitiza huruma, haki na ufufuaji wa jamii zilizoelemewa na madeni yasiyo ya haki.

VATICAN CITY, Vatican

Baba Mtakatifu Fransisko amesema kuwa mateso na mahangaiko ya mwanadamu, ni zawadi ya matumaini na uaminifu wa Mungu katika Fumbo la Pasaka, na kwamba upendo wa Mungu daima utawaandama waja wake hata wakati wa majaribu na vikwazo katika maisha yao.
Papa alitoa ujumbe huo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Siku ya 33 ya Wagonjwa Duniani mwaka 2025, iliyoadhimishwa mjini Vatican, siku ambayo ilianzishwa Mei 13 mwaka 1992, na kuadhimishwa kwa mara ya kwanza kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Lourdes nchini Ufaransa, mnamo Februari 11 mwaka 1993.
Maadhimisho ya Siku ya Wagonjwa kwa ngazi ya kijimbo yaliyoadhimishwa mwaka huu wa 2025, yananogeshwa na kauli mbiu isemayo, “Na tumaini halitahayarishi, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu,” huku Baba Mtakatifu akiwaalika watu wote wa Mungu kuwa Mahujaji wa Matumaini.

VATICAN CITY, Vatican

Wanajeshi na Polisi wametakiwa kutambua kwamba wameitwa na Mungu ili kutetea wanyonge, kulinda waamini, kuhamasisha watu kuishi kwa amani, pamoja na kuendeleza haki na amani kila mahali.
Hayo yalisemwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Baba Mtakatifu Fransisko katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Vikosi vya Wanajeshi, Polisi na Usalama, aliyoiadhimisha mjini Roma hivi karibuni.
“Ni nani bora kuliko ninyi, wanajeshi na polisi wapendwa, wavulana na wasichana, wanaweza kushuhudia vurugu na kusambaratika kwa nguvu za uovu zilizopo ulimwenguni? Mnapigana nao kila siku. Kiukweli mmeitwa kutetea wanyonge, kulinda Waamini, kuhamasisha kuishi kwa amani kwa watu…
“Kila mmoja wenu anafaa kwa nafasi ya ulinzi, ambaye anatazama mbele sana, ili kuepusha hatari na kuendeleza haki na amani kila mahali. Ninawasalimu ninyi nyote kwa upendo mkuu, Ndugu wapendwa, ambao mmefika Roma kutoka sehemu nyingi za dunia kusherehekea Jubilei yenu maalum…..

DAR ES SALAAM

Na Dk. Felician B. Kilahama

Mitihani ya kuhitimisha Kidato cha Nne, Tanzania (CSEE) ilifanyika Novemba 11 hadi 29, 2024.
Matokeo yakatangazwa rasimi Januari 23, 2025 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (National Examinations Council of Tanzania: NECTA) Dk. Said Mohammed kupitia hafla na Waandishi wa Habari.
Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa NECTA, ilionyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia tatu (3) kutokana na watahiniwa wengi kufaulu.
Hiyo inamaanisha kuwa kati ya watahimiwa 516,695, kati ya hao watahiniwa 477,262 wamefauli kwa madaraja: I, II, III na IV; ikiwa ni ufaulu wa asilimia 92.37 kulinganisha na matokeo ya mitihani ya 2023 yenye ufaulu wa asilimia 89.36 tu.
Kadhalika, ufaulu kwa madaraja ya I, II na III ni watahiniwa 221,952 sawa na asilimia 43, wakati mwaka 2023 walikuwa watahiniwa 197,426 sawa na asilimia 37.4 tu.
Vile vile, matokeo yameonyesha kuwa waliopata daraja la nne (iv) pamoja na waliopata alama (sufuri) wamepungua kulinganisha na matokeo ya mwaka 2023; hivyo kuashiria ongezeko la asilimia 5.6 wa ubora wa kufaulu.
Hata hivyo, Katibu Mtendaji, NECTA alibainisha kuwa kwa matokeo ya mwaka 2024, watahiniwa 67, NECTA imelazimika kufuta matokeo yao kutokana na udanganyifu wakati wakifanya mitihani.

DAR ES SALAAM

Na Alex Kachhelewa

Viongozi wa Matifa ya Afrika Mashariki (East African Community: EAC) na wale wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Southern Africa Development Community: SADC), walikutana hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika Mkutano Maalumu kuhusu kusaka suluhu ya mzozo wa vita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mzozo huo ni kati ya Majeshi ya Serikali ya DRC dhidi ya Vikosi vya Waasi wa Movement For March 23- au maarufu kama M23, wanaosadikiwa kuuteka Mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Katika mkutano huo ambapo Rais wa DRC Felix Tshisekedi Shilombo, yeye alishiriki kwa njia ya Mtandao, Viongozi hao walifanya maamuzi yatakayosaidia kurejesha amani  katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), iliyogubikwa na mzozo wa muda mrefu zaidi kuwahi kushuhudiwa.
Mkutano huo uliwakaribisha viongozi hao chini ya Mwenyeji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, uliohudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa wanachama wa EAC na SADC,  ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa EAC, Rais William Ruto wa Jamhuri ya Kenya, na Mwenyekiti wa SADC, Rais Emmerson Mnangagwa wa  Jamhuri ya Zimbabwe,  hapakuwapo Rais wa Congo DRC Felix Tshisekedi, ambaye alishiriki kwa njia ya mtandao.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Joseph Mayanja, maarufu kwa jina lake la jukwaani, Jose Chameleone, ni mmoja wa waanzilishi wa muziki wa Uganda, ni mwanamuziki maarufu wa Afrobeat nchini Uganda akiwa na nyimbo nyingi zilizovuma kwa jina lake, akiimba muziki wake kwa kutumia mchanganyiko wa lugha za Luganda, Kiingereza na Kiswahili.
Mwanamuziki huyo mwenye talanta nyingi, alitoa rekodi yake ya kwanza na Ogopa DJs nchini Kenya mwaka 1996, kwa kutoa wimbo wake wa kwanza, ‘Bageya’, ambao alimshirikisha msanii wa Kenya, Redsan, wimbo ambao ulimpa mafanikio makubwa.
Jose Chameleone alizaliwa Aprili 30, 1979 mjini Kampala, nchini Uganda. Wazazi wake ni Gerald Mayanja (Baba), na Prossy Mayanja (Mama), lakini pia ana ndugu zake wanaojulikana ambao ni Douglas Mayanja a.k.a Weasel - Msanii wa Goodlyfe Crew, na msanii wa solo Pius Mayanja a.k.a Pallaso - Msanii wa muziki Henry Kasozi - Mkurugenzi Mtendaji wa Fling Fire cloth line marehemu Emmanuel Mayanja, a.k.a AK47.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Imepita miaka 21 sasa tangu kocha Jose Mourinho kupewa jina la utani la ‘Special One’, likiwa na tafsiri ya Mtu Maalum.
Jina hilo limekuwa kubwa duniani na hivyo kumtambulisha vilivyo katika medani ya soka.
Picha lilianzia mwaka 2004 ambapo Chelsea ilimtambulisha kwa waandishi wa habari kocha wao mpya, Jose Mourinho.
Raia huyo wa Ureno alijiunga na Chelsea akitoka kuwa bingwa wa Ulaya akiwa na FC Porto.
Waandishi wa habari wakamuuliza kama anaweza kurudia kufanya alichokifanya akiwa FC Porto, yaani kuahidi ubingwa na kuuchukua.

MANCHESTER, Uingereza
Tangu amepoteza mara mbili mfululizo dhidi ya Zhilei Zhang mwaka 2023, Joe Joyce, raia wa Uingereza, hajakaa sawa licha ya kushinda pambano lililofuata dhidi ya Kash Ali, lakini bado alipoteza mbele ya Derek Chisora.
Aprili 05 mwaka huu, Joe Joyce atamkabili Mwingereza mwenzake Dillian Whyte jijini Manchester, lakini kabda ya pambano hilo, Joe ambaye amewahi kuwa bingwa wa World Boxing Organisation (WBO) Interim, atapasha misuli kwa pambano la raundi nane dhidi ya Patrick Korte wa Ujerumani, Machi mosi.

DAR ES SALAAM

Na Nicolaus Kilowoko

Kufuatia kuwa na mwendelezo mzuri tangu alipojiunga na klabu ya soka ya Simba, kocha raia wa Afrika Kusini Fadlu Davis, imeelezwa kuwa ameanza kuufatiliwa na viongozi wa juu wa klabu ya soka ya USM Alger, kutoka nchini Algeria.
Habari ambazo Tumaini Letu imepekua na kuzidaka zinaeleza kuwa matajiri hao kutoka Algeria wanataka kuvunja kibubu kwa ajili ya kuhakikisha kocha huyo wanamtwaa, ili akawasaidie kwenye Ligi yao pamoja na michuano ya Klabu Bingwa Afrika, kitu ambacho kinaonekana kuwachanganya Simba.
Ikumbukwe hata kocha Sead Ramovic aliwaponyoka Yanga hivi karibuni baada ya matajiri wa Belouizdad kuweka pesa nyingi mezani, dau ambalo inaelezwa liliwawia vigumu Yanga kumbakisha.

Mbunge wa Jimbo la Njombe, Deo Mwanyika (wa nne katikati), akipokea Kombe kutoka kwa nahodha wa timu ya Utalingoro, Adalbert Ngole, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi katika Mashindano ya Kombe la Ng’ombe kwa kuichapa timu ya Uwemba 1-0 mshindi alipata zawadi ya ng’ombe. Kushoto kwa Mbunge ni Diwani wa Kata ya Utalingoro, Erasto Mpete. (Picha kwa hisani ya Bertold Njawike)